The House of Favourite Newspapers

Nyumba ya Michael Jackson Yauzwa kwa Bil. 51

0

NYUMBA aliyokuwa akiishi mfalme wa muziki wa Pop duniani, marehemu Michael Jackson, imeuzwa kwa bilionea Ron Burkle kwa  Dola za Marekani mil. 22 ambazo ni sawa na bil. 51 za Tanzania.

 

 

Burkle, ambaye alikuwa rafiki wa zamani wa Jackson, hivi karibuni aliinunua nyumba hiyo  iliyoko Los Olivos, California, Marekanim ambapo msemaji wake alisema nyumba hiyo imejengwa  katika shamba lenye ekari 2,700 .

 

 

Mwanamuziki huyo alilinunua jumba hilo mwaka 1987, wakati ambao alikuwa anafanya vizuri kwenye muziki wa Pop kupewa jina la Mfalme wa Pop.

 

Alibadilisha jumba hilo na kuwa eneo la burudani, akijenga eneo la kufuga wanyama mbali na ukumbi wa chini ya ardhi ambapo aliwafurahisha watoto na familia zilizokuwa zinamtembelea.

 

Miaka 1990 na 2000, jumba hilo lilichunguzwa sana kutokana na madai ya udhalilishaji watoto kingono dhidi ya mfalme huyo wa Pop.

 

Jackson alikana madai hayo yaliyowasilishwa na kiongozi wa mashtaka wa eneo la Santa Barbara akisema kwamba alitumia nyumba hiyo kuwafurahisha watoto na michezo mbalimbali.

 

Mwaka 2005, Jackson alishtakiwa na kuachiliwa huru kwa madai kwamba alimnyanyasa mvulana wa miaka 13 katika jumba hilo.

 

Jackson hakurudi tena katika kasri hilo na miaka minne baadaye mwezi Juni 2009, alifariki katika nyumba yake nyingine mjini Los Angeles, baada ya kukumbwa na mshtuko wa moyo uliotokana na kunywa dawa kupitia kiasi.

Leave A Reply