The House of Favourite Newspapers

Obama Diwani wa Kihistoria Kata ya Mabwepande

0
Diwani Obama (aliyesimama) akizungumza kwenye mkutano huo.

Wakazi wa Kata ya Mabwepande Wilaya ya Kinondoni Dar, wametoa la moyoni kwa kummwagia sifa hadharani diwani wao, Muhajirina Kassim Obama ambaye ameanza msimu wake mpya kwa kupania kumaliza kero za wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi na mingineyo ambayo imekuwa sugu kwenye kata hiyo.

Obama alimwagiwa sifa hizo kwenye mkutano wake wa kusikiliza kero za wananchi wake uliofanyika Bunju A umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza kumsikiliza.

Diwani huyo alikuwa akisikiliza kero za wananchi hao ambazo zilizo ndani ya uwezo wake alizimaliza palepale na zingine aliahidi kuzimaliza baada ya muda na kamati yake na zilizo juu uwezo wake aliwaahidi wananchi hao kuzipeleka kwa viongozi wake wa juu na kuwaahidi nazo kuzimaliza.

Mmoja wa wananchi akionesha nyaraka zake.

Wakizungumza baada ya mkutano huo baadhi ya wananchi walisema diwani huyo ni wa kihistoria kwenye kata hiyo kwani katika kipindi chote cha maisha yao kwenye kata hiyo hakuwahi kutokea kiongozi wa aliyekuwa akiwasikiliza kero zao na kuzimaliza kama alinavyofanya yeye.

“Mimi ni mkazi wa hili eneo kwa zaidi ya miaka kumi sasa lakini katika kukaa kwangu miaka yote hiyo sijawahi kusikia kiongozi yeyote akiitisha kikao cha kusikiliza kero za wananchi.

Mkutano ukiendelea.

“Huyu ndiyo diwani wa kwanza kufanya hivi  ukweli ni lazima tumpongeze maana haya maeneo yamekuwa sugu na migogoro na tulikuwa hatujui tuimalizeje,” alisema mwananchi huyo.

Mkutano huo ulimalizika kwa mayowe ya kumshangilia wananchi wakilipuka kwa mayowe ya ya furaha wengine wakitaka kumbeba.

Leave A Reply