The House of Favourite Newspapers

Ofa ya Ronaldo Kucheza Saudi Arabia Inatisha, Mshahara Wake ni Kufuru

0
Nyota wa Timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo

NYOTA wa zamani wa Manchester United, Real Madrid na Juventus Cristiano Ronaldo amepokea ofa ya kutisha kutoka klabu ya Al Nass rya nchini Saudi Arabia yenye thamani ya paundi milioni 200 ikiwa na mkataba wa miaka miwili na nusu ili nyota huyo atimkie katika Ligi Kuu ya nchini humo.

 

Ronaldo ambaye mkataba wake na Manchester United umevunjwa hivi karibuni kwa sasa ni mchezaji huru akiwa na timu yake ya taifa ya Ureno akishiriki mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar ambapo hadi sasa timu yake imefuzu katika hatua ya 16 ya mashindano hayo.

Cristiano Ronaldo kwa sasa yupo na Timu ya Taifa ya Ureno kwenye mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar

Kiasi cha paundi milioni 200 ni kwa kila msimu ambapo haijawekwa wazi Kama kitita hicho kitahusisha pia haki za matangazo, kutokana na Cristiano Ronaldo kuwa si mchezaji mzuri pekee lakini ni moja kati ya wanamichezo wenye mvuto mkubwa akiwa na mikataba minono ya matangazo.

 

Kwa sasa taarifa zimebainisha kuwa wakala wa Cristiano Ronaldo, Jorge Mendes anafuatilia kwa karibu ofa hiyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia vipengele mbalimbali vya mkataba huku Cristiano Ronaldo akiweka akili yake katika kuisaidia timu yake ya taifa ya Ureno kutwaa Kombe la Dunia ingawa Habari pia zimebainisha kuwa tayari Ronaldo anayo taarifa juu ya Ofa hiyo na huenda akaipa kipaumbele.

Leave A Reply