The House of Favourite Newspapers

Ofisa Benki Atumbuliwa kwa Kulala na Wanaume 200

WANANCHI nchini Zambia wameshangazwa na habari kwamba ofisa mmoja mwanamke wa Benki ya Taifa ya Biashara ya Zambia (ZANACO), amesimamishwa kazi na menejimenti ya benki hiyo kwa kudai kufanya ngono na wanaume 200 kwa kuwaahidi kuwapatia kazi na kupitisha maombi yao ya mikopo katika  benki hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti la Zambian Observer, wengi wa wanaume hao wamedaiwa kuwa ni wateja wa benki hiyo na waliokuwa wakitafuta ajira, na hivyo kujikuta kitandani wakifanya ngono na Mutale Winfridah mwenye umri wa miaka 39 na ambaye alikuwa Ofisa Mwandamizi Mtendaji katika tawi la Benki hiyo huko Kitwe.

Tukilo hilo limegundulika baada ya wanaume kumi kufikisha malalamiko yao katika menejimenti ya benki hiyo kwamba mama huyo alikuwa ‘akiwatongoza’ ili kufanya naye ngono.

 

Winfridah bado hajaolewa kwa kile kinachosemekana anataka kwanza kwenda kujiendeleza kimasomo.

Tukio lenye kushabihiana na hilo lilitokea nchini Uganda mwaka jana ambapo ofisa wa Chuo Kikuu cha Makerere, Edward Kisuze,  alisimamishwa kazi kwa kutaka kumbaka mwanafunzi wa kike, Rachael Njeri,  aliyekwenda chuoni hapo kupata hati za matokeo ya mitihani yake.

Mwanamke huyo alibahatika kumpiga picha ofisa huyo wakati akimbembeleza na akai-posti katika mitandao ya kijamii.

Comments are closed.