The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kujifungua…. Chumba Mtoto wa Tanasha Bab’kubwa

DAR ES SALAAM: Ikiwa imepita siku moja tangu ajifungue mtoto wa kiume na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, chumba cha mtoto wa mtangazaji ambaye pia ni mchumba wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Tanasha Donna Oketch ambacho ni baab’kubwa.

TUJIUNGE ‘USHUANI’

Kwa mujibu wa mtu wa karibu na familia ya Diamond au Mondi, mara baada ya Tanasha kujifungua alfajiri ya Jumatano katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar, wamemtengea chumba maalum katika ‘white house’ ya rais huyo wa Wasafi Classic Baby (WCB) iliyopo Mbezi- Beach jijini Dar kwenye Ufukwe wa Bahari ya Hindi.

Kwa mujibu wa mtu huyo, chumba hicho tayari kimejazwa vitu mbalimbali kutoka Afrika Kusini ‘Sauz’, Dubai na London nchini Uingereza.

ETI KIMEPAKWA MADINI

Chanzo hicho kilinyetisha kwamba, pamoja na vitu vingine, lakini chumba hicho kina kitanda spesho cha mtoto huyo ambacho kimepakwa madini (hakutaja ni madini ya aina gani).

“Wewe fikiria, kama alipokuwa akiishi mwanzoni kule Madale (jijini Dar) toileti kwake ameweka vitu vya madini inashindikana nini kwa mtoto wake aliyezaliwa kumuwekea?

DAZENI KWA DAZENI

“Mbali na hivyo, kuna vitaulo, nepi, pempasi, vitambaa na vichupi vya mtoto dazeni kwa dazeni, mafuta na poda za mtoto, tishu na pini ambavyo vimejazwa kwenye vikabati maalum ambavyo haviingizi vumbi.

“Pia chumba hicho kina midoli mizuri ya mtoto iliyopamba masofa yaliyopo ndani ya chumba hicho ambacho hakiruhusiwi mtu mwingine kuingia zaidi ya Tanasha na Diamond,” kilisema chanzo chetu hicho.

GHARAMA MIL. 10

Sosi wetu huyo wa kuaminika alisema kwamba ukiacha kitanda, masofa, gharama ya utengenezaji, vikokoro vyote vinagharimu zaidi ya shilingi milioni 10 za Kitanzania.

“Unajua vitu ni vingi na jamaa (Diamond) huwa ananunua kila kukicha ‘so’ sidhani kama anaweza akawa na ‘figa’ kamili ila kwa nguo na vitu vingine vidodovidogo si chini ya milioni kumi,” alisema sosi huyo kwa sharti la kutochorwa gazetini kwa kigezo kuwa si msemaji wa familia.

BABY SHOWER KUJAZIA

Chanzo kiliendelea kunogesha kuwa, mbali na Diamond kununua vitu vingi nje ya nchi, pia vingine ambavyo amezawadiwa Tanasha katika baby shower yake hivi karibuni vitakuwepo katika chumba hicho.

“Inategemea sasa, ataangalia kama vile ambavyo amepewa kwenye baby shower yake navyo vitumike kwa kipindi hiki au atumie kwanza ambavyo amenunuliwa nje ya nchi,” chanzo kiliweka nukta.

MTOTO WA NNE

Mtoto aliyejifungua Tanasha anakuwa wanne baada ya kuwa nao wengine wawili kutoka kwa mwanamama mjasiriamali Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ ambao ni Tiffah na Nillan. Mwingine mmoja amezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto aitwaye Dylan.

Stori: Imelda Mtema, Ijumaa

Comments are closed.