Kartra

Ofisi za CHADEMA Zachomwa Moto – Video

Usiku wa kuamkia leo Oktoba 13, 2021 ofisi ya CHADEMA jimbo la Tunduma, Mkoa wa Songwe imechomwa moto na watu wasiojulikana, wananchi pamoja na kikosi cha zimamoto walifanikiwa kuzima moto huo.


Taarifa zinaeleza kuwa vitu kadhaa vya ofisi hiyo vimeteketea kwa moto huo huku chanzo chake kikiwa hakijafahamika.

RPC Mkoa wa Songwe Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kuchomwa moto baadhi ya nyaraka mbalimbali ambazo zilikuwemo ndani ya ofisi hyio ya CHADEMA.


Toa comment