The House of Favourite Newspapers

OFM yatumbua jipu Hospitali ya Palestina

0

IMG_1749 Taa za chooni zikiwa haziwaki.

Chande Abdallah na Boniface Ngumije
Kwa mara nyingine, kitengo maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kimekuta majipu na kulazimika kuyatumbua katika Hospitali ya Palestina, iliyopo Sinza Dar inayokabiliwa na tatizo la nishati ya uhakika ya umeme.

Hospitali hiyo ambayo imepanda hadhi na kuwa ya Wilaya ya Kinondoni, kwa muda mrefu imekosa huduma ya uhakika ya umeme, hali inayosababisha wagonjwa kupata tabu wawapo eneo hilo.

IMG_20160105_163409

Eneo la chooni ambalo ni giza.

Wakizungumza na OFM kutokea hospitalini hapo, wagonjwa walisema mara kwa mara hulazimika kusubiri huduma ikiwa umeme utakatika.

“Mimi ningependa sana muende pale Palestina ili msaidie, maana kama wagonjwa walitoa taarifa za ubovu wa vifaa pale Muhimbili na kweli rais akawasaidia basi na huku kwetu iwe hivyo, hata jenereta liletwe lingine.

“Sikatai, kuna huduma nzuri na majengo mazuri lakini tatizo ni umeme, kuna wakati unaenda kule vyooni unakuta giza tupu licha ya kwamba umeme upo,” alisema mmoja wa wagonjwa.

IMG_20160105_163314OFM ilifika hospitalini hapo na baada ya uchunguzi, ilibaini ukweli wa madai hayo, kwani taa ambazo zipo vyooni na baadhi ya maeneo mengine haziwaki huku genereta pia likiwa ni tatizo.

Aidha, OFM ilibaini kutowaka kwa taa za vyooni ambazo huwa muhimu kwa wagonjwa pindi wanapotakiwa kuchukua baadhi ya vipimo kama vile choo kidogo na kikubwa.
Pia mashine ya kufua umeme wa jua ‘solar panel’ iliyofungwa juu ya paa la hospitali hiyo, haina msaada kwani inadaiwa tangu ifungwe haizalishi umeme.

OFM ilimtafuta Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Azizi Msuya ambaye alisema umeme hospitalini hapo ni tatizo linalochangiwa na uwajibikaji mdogo wa viongozi.IMG_2251

Lango la kuingilia hospitalini hapo.

“Hapa kuna uzembe, leo tu nimetoka kuzungumza na viongozi wa pale, wanataka niwamalizie gharama za solar panel mafundi waliokuwa wanashughulikia suala hilo wakati hali ya umeme hairidhishi, siwezi kuwa msimamizi wa watu wazembe hata siku moja,” alisema daktari huyo.

Leave A Reply