The House of Favourite Newspapers

Okwi aibeba familia kuja nayo Bongo

0

 

MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi, raia wa Uganda, ameamua kuja kivingine katika kutekeleza majukumu yake ya uwanja ambapo ameahidi kushuka na familia yake ili iweze kumsapoti kwa karibu pindi atakapoanza kutekeleza majukumu ya kibarua chake.

 

Okwi aliyefunga ndoa kipindi cha mwaka 2012 kabla ya kuondoka Simba na baada ya hapo kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike, amesema anakuja na familia kwa kuwa kipindi hiki ana uhakika wa nyumba ya kuishi tofauti na ilivyokuwa mwanzo wakati akiitumikia klabu hiyo huku maisha yake yote akiishi hoteli.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Okwi ametanabaisha kwamba kwa kuwa amejipanga kuja kupiga kazi na kuhakikisha timu yake inafanya vizuri, atatua nchini akiwa na familia yake yaani mke na mtoto wake ili waweze kumpa sapoti kubwa kwa kuwa anatamani kutimiza majukumu yake huku familia ikiwa inamshuhudia.

 

“Ujue maisha marefu niliyoitumikia Simba sikuwa na mke maana nilikuwa sijaoa, hivyo hata nilipoenda kucheza nje sikupata nafasi ya kwenda naye kwa kuwa tu alikuwa mjamzito lakini hata alipojifungua sikuweza kumsafirisha kwa sababu mtoto alikuwa bado mdogo.

 

“Kutimiza furaha yangu kipindi hiki nitakuja kuishi naye ili aone kwa karibu maisha yetu tunapokuwa nje ya nyumbani maana uwepo wake naamini kabisa utakuwa ni hamasa kubwa kwangu kwani nitakuwa na muda mwingi wa kufikiria familia maana hata mtoto wangu atakuwa karibu yangu,” alisema Okwi.

 

Musa Mateja | Dar es Salaam

VIDEO: BABA AINGILIA VITA YA GOLIKIPA MANYIKA NA MANULA SIMBA

Leave A Reply