The House of Favourite Newspapers

Ombaomba Bado Wanatesa Jiji la Makonda

maktabaOmbaomba ambao ni wasichana wadogo, wakipita kuomba katika magari yaliyokuwa katika foleni jijini Dar.

LICHA ya mara kadhaa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  kuwapigia kelele ombaomba akiwataka waondoke jijini Dar es Salaam,  jambo  hilo limeonekana kupuuzwa na wahusika baada ya kamera yetu leo kuwanasa ombaorasmi.Ombaomba hao  walinaswa wakiwa katika Barabara ya Bibi mba ambao ni watoto  wakiendelea na kazi yao hiyo isiyo rasmi.

Ombaomba hao  walinaswa wakiwa katika Barabara ya Bibi Titi  karibu na Maktaba Kuu ya Taifa wakiomba katika magari yaliyokuwa kwenye foleni yalipokuwa yamesimamishwa na taa za kuongozea magari.

Cha ajabu ni kwamba, kati ya hao ombaomba, wengi wao ni watoto wanaokadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka tisa mpaka 12 ambao kwa kawaida walitakiwa kuwa shule, lakini pia mazingira wanayotumia kuomba ni hatari kwao kwani ni barabarani.

Tangu awe mkuu wa mkoa huu, Makonda amekuwa akipambana nao kila mara lakini ombaomba hao wamekuwa hawataki kuitikia wito wake wa kuwataka waondoke mitaani na kurejea kwao ili kuweza kuhudumiwa na jamii zao na mamlaka za huko.

Na Denis Mtima/GPL

Comments are closed.