The House of Favourite Newspapers

Omog Ndiyo Basi Tena Kwa Nyoni

0
Erasto Nyoni.

BEKI kiraka wa Simba, Erasto Nyoni, amefanikiwa kumteka akili kocha mkuu wa timu hiyo, Mcameroon, Joseph Omog baada ya kufanikiwa kuandika rekodi ya pekee ndani ya kikosi hicho.

Nyoni ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea Azam FC, ameandika rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza ndani ya timu hiyo kutengeneza nafasi nyingi za kufunga msimu huu, kuliko wachezaji wengine wote.

Katika mechi tatu alizoitumikia timu hiyo, Nyoni ametengeneza nafasi za mabao manne kati ya 12 ambayo Simba imefunga mpaka sasa jambo ambalo limepokelewa kwa mikono miwili na Omog.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Omog alisema kuwa mpaka sasa Nyoni ndiye mchezaji aliyetengeneza nafasi nyingi za mabao kikosini hapo kuliko mchezaji mwingine licha ya kucheza nafasi ya beki wa pembeni.

Alisema katika mabao 12 ambayo timu hiyo imefunga mpaka sasa Nyoni ametengeneza manne, jambo ambalo si jepesi kufanywa na mchezaji anayecheza nafasi kama yake.

“Hakika Nyoni ameonyesha kuwa ni mchezaji wa kipekee kwani tangu amejiunga nasi amekuwa akifanya vizuri kila siku jambo ambalo linawashangaza wengi wakiwemo viongozi wetu.

“Katika mechi tatu za ligi alizocheza amefanikiwa kufunga bao moja lakini pia ametengeneza nafasi nne za kufunga, alitengeneza nafasi za mabao mawili dhidi ya Ruvu Shooting, lakini pia tulipocheza na Mbao FC, nampongeza kwa hilo,” alisema Omog na kuongeza:

“Mtu kama huyo siyo rahisi akakosa nafasi ya kucheza kutokana na uwezo wake mkubwa anaouonyesha uwanjani.”

Mpaka kufikia sasa Simba ndiyo inayoongoza kwa kuwa na mabao mengi ya kufunga kuliko timu nyingine zote zinazoshiriki ligi kuu.

 Sweetbert Lukonge, Dar es salaam

 

SIRI Imefichuka Baada ya Kushushwa kwa Bilionea Yanga wa Kulipa Mishahara

Leave A Reply