The House of Favourite Newspapers

Ooh…madam martha!-2

1

Alikaa kwa kujiachia kiasi kwamba, kanga ilijiachia kidogo, sehemu kubwa ya mapaja yake ikawa wazi, John akachungulia kwa mbali na kugeuka kuangalia mlango mkubwa alioingilia…

“Hapa ndiyo kwangu John, lakini ulikuwa hujawahi kufika wewe!”
“Niliwahi kuja siku moja na Daudi, ulimtuma kitabu cha Sayansi…”

TAMBAA NAYO SASA…
“Oooh! Nakumbuka, sawasawa,” alisema Madam Martha huku akiangalia pembeni kisha akamwangalia John, wakakutana macho, madam Martha akaachia tabasamu na kusema…

“Unajua John, ni kweli kabisa nimeamini kuku mgeni hakosi kamba mguuni…”
“Kwa nini madam..?”

“Siku ya kwanza nilipokuona tu, nilijua kwa vyovyote vile huwezi kuwa mzawa wa hapa Katoro,” alisema Madam Martha huku akiiweka sawa khanga yake iliyokuwa imeanza kutambaa chini upande wa mbele.

Hali hiyo ilisababisha sehemu kubwa ya paja la kushoto kubaki wazi kwa mita chache kutoka kwenye goti.

“Mmh! Kawaida sana mwalimu, lakini hujakosea sana,” alijibu John lakini safari hii kwa sauti ya mawimbi na mkwamo kidogo.

“Hiyo tabia ya usafi na utanashati umeirithi kwa mtu au ni ya kwako mwenyewe?” aliuliza Madam Martha lakini si kwa kumaanisha alichokiuliza bali ni kwa lengo la kupoteza muda kwani swali lake halikuwa na uhalisia wowote.

Ikafika mahali, si John wala Madam Martha aliyemsemesha mwenzake zaidi ya kutazamana na kuruhusu macho yazungumze.

“Ina maana kweli huyu anaweza akawa hajajiongeza ni kwa nini nimemuita hapa kwangu?” aliwaza moyoni Madam Martha…

“Kha! Sasa kama ameniita mbona hataki kunieleza chochote au ni yaleyale kama wasichana wengine kushoboka na utozi wangu?” huyu sasa alikuwa ni John akiwaza yake moyoni.

“Eeh, nilisahau jamani… unakunywa nini John?” alikurupuka Madam Martha na kujibalaguza kwa swali hilo, lakini tayari alikuwa hoi kihisia juu ya mwanafunzi wake huyo mtanashati kupindukia.

“Mh! Chochote tu madam ila isiwe kilevi,” alijibu John kwa mkato huku akikimbiza macho yake pembeni.Haraka Madam Martha aliinuka na kulifuata friji lililokuwa pembezoni mwa sebule hiyo iliyokuwa imejaa samani na mazagazaga mengine, lakini mengi yakiwa mapambo kama midoli na wanyama wa kuchonga, tembo na twiga.

Wakati anainuka, kwa nyuma khanga ikawa imejishika au kujibana kwenye wowowo na kumfanya sehemu hiyo kujichora vyema umbo la Madam Martha.

Kwa kuwa John ni mtoto wa mjini, akawa anajua ni kwa nini Madam Martha aliamua kujitega vile mbele yake, moyoni akawa na wakati mgumu wa namna gani ataweza kuwa jasiri mbele ya mwalimu wake huyo wa somo la Bailojia.

Hata hivyo, kwa kuwa Madam Martha naye ni mtoto wa mjini, kwa muda ambao alikuwa ameutumia kuzungumza na John, tayari alishajua ni kijana wa aina gani ingawa alionekana kutoutumia vyema utanashati wake, lakini moyoni alidhamiria kumnasa.

Sababu za kumtaka John zilikuwa nyingi lakini kwanza, kutokana na kupata historia yake kuwa ni kijana wa Dar es Salaam aliyehamia Katoro kwa uhamisho wa baba yeke, hivyo ni mtu wa hadhi yake japokuwa alimshinda kwa mbali umri na pia alikuwa ni mwanafunzi wake, yote hakuyajali sana zaidi ya kutaka kusuuza kiu ya moyo wake.

Sasa ikawa wakati anafungua friji, Madam Martha akapania kufanya makusudi. Akawa mara ainame, mara abinuke na wakati mwingine achuchumae ule mkao wa mtego na kulitingisha kimtindo wowowo lake lililokuwa bado halijakauka maji…

Huku nyuma, hali ya John sasa ikawa tete, kuna wakati akajisahau kuwa aliye mbele yake ni mwalimu wake tena wa somo nyeti na muhimu.
Kufikia hapo, tayari akawa John ngangari kama siyo ngunguri.

Madam Martha alitoka na juisi ya embe na kumpa John. Kwa kuwa kochi alilokuwa amekaa John lilikuwa la watu wawili, Madam Martha akaamua kukaa kabisa sambamba na mwanafunzi wake huyo.

Ikatokea wakati akikaa, akajikuta mguu mmoja ukiteleza kidogo na kumwegemea John kwa upande mmoja wa paja. Sasa ikawa John anasikilizia kiaina joto la mwalimu wake huku mwalimu huyo akifaidi manukato mazuri aliyokuwa amejipulizia mwanafunzi huyo.

Bila kusema chochote, wote wawili kila mmoja moyoni akamtamani mwenzake abaki vilevile.

Ilifika mahali, Madam Martha akazidi kujisogeza kwa John bila kujizuia akawa akasogeza uso wake karibu kabisa na kifua cha mwanafunzi huyo, aibu za mtu na mwalimu wake zilishamtoka kichwani isipokuwa kwa upande wa John hali hiyo ilijitokeza akilini mara kwa mara.

Kuona hapati upinzani wala katazo lolote, Madam Martha ambaye ugonjwa wake mkubwa ni wanaume watanashati, aliupeleka mkono kifuani kwa denti wake na kuanza kuuchezesha kiaina huku akikisifia kifua kipana cha John.

Ikawa wakati akijiandaa kupiga hatua zaidi huku John akiwa ameduwaa kama aliyepigwa na shoti ya umeme, ghafla mlango ulifunguliwa bila mtu kubisha hodi.

Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kwenye gazeti hilihili, Jumanne ijayo.

1 Comment
  1. Jabu says

    Its so hot!

Leave A Reply