The House of Favourite Newspapers

Shoga; Sikukuu ukiachwa solemba uzembe wako!

0

Kabla sijaanza kuzungumzia mada ya leo, napenda kuwatakia afya njema wenzetu wanaoumwa, waliofiwa au walio kwenye matatizo mbalimbali, Mungu awaepushe na masaibu hayo na kuwapa faraja.

Shoga yangu, kama unavyoelewa kwamba siku si nyingi kutakuwa na Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya ambazo ni za kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka wa 2016.

Sikukuu hizo zina umuhimu wake kwa sababu Wakristo wanakumbuka siku ya kuzaliwa Mwokozi wao Bwana Yesu huku wakiungana na watu wa dini zingine na wasio na dini kusherehekea Mwaka Mpya.

Wengi wakati huo hutathmini mafanikio waliyoyapata kimaendeleo na hata kiuhusiano kwani kama wewe na mumeo, mchumba au mpenzi wako mmeweza kumaliza mwaka bila migogoro basi ni jambo la kumshukuru Mungu.

Nasema hivyo kwa sababu, wapo wenza ambao unaposoma makala haya wameachana kwa kukashifiana na wengine wamepeana vilema na hata kuuana kwa sababu ya mapenzi.

Kama wewe na mwenza wako hamkupata kikwazo katika ndoa au uchumba wenu ni vyema kusherehekea sikukuu hizo pamoja kwa kutoka ‘out’ na familia yenu kwani hayo ndiyo mapenzi.

Hata hivyo, wakati huo wa sikukuu kama hutakuwa makini ndiyo siku ambazo wababa wengi huzitumia kuwasaliti wenzao kwa kwenda kula sikukuu na nyumba ndogo.

Ikitokea mumeo siku hiyo akakuacha nyumbani na kwenda kula sikukuu na nyumba ndogo huo utakuwa uzembe wako kwa sababu utamruhusuje atoke peke yake?
Nasema utakuwa uzembe wako kwa sababu siku za sikukuu hizo za kufungia mwaka wanandoa na wapendanao wengine huzitumia kusameheana na kujenga penzi lao sasa inakuwaje mumeo akutoroke na kwenda kwa mchepuko? Kuwa makini!

Leave A Reply