The House of Favourite Newspapers

Overmars; Alikulia Kwenye Mashamba ya Viazi, Akawa Staa wa Dunia

marc-overmars3UKICHUNGULIA kwenye kikosi cha Ar­senal kilichotwaa ub­ingwa wa Premier 1997-98, ndani yake utakutana na sura ya Mholanzi matata, Marc Overmars.

Overmars, aliyezaliwa Machi 29, 1973, utakumbuka jinsi al­ivyokuwa winga mwenye kasi na mbinu nyingi za kiufundi za kumtoka mpinzani.

Umaarufu wa Overmars, 43, ulianza akiwa na kikosi cha Ajax chini ya kocha Louis van Gaal ambacho alikisaidia kut­waa mataji matatu ya Ligi Kuu ya Uholanzi (Eredivisie) kati ya 1994 na 1996 pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1995.

marc-overmars1Desemba 1995, Overmars alipata changamoto kubwa, kwani alipata majeraha ya goti yaliyomweka nje ya uwanja kwa miezi nane.

Mwaka 1997, alijiunga na Arsenal lakini mwanzoni ki­wango chake kilizodolewa na kupondwa vibaya na wacham­buzi pamoja na mashabiki. Hata hivyo, katikati ya msimu wake wa kwanza, Overmars alijikuta akiwa mtu muhimu na kuisaidia klabu yake kutwaa ubingwa wa Premier na Kombe la FA kwa mpigo. Alifunga bao la ushindi dhidi ya wapinzani wao Man­chester

United katika ushindi ambao ulitengeneza njia ya ub­ingwa, pia ndiye aliyefunga bao la kwanza dhidi ya Newcastle katika fainali ya FA.

Mwaka 2000, alijiunga na Barcelona kwa dau la pauni mil­ioni 25 na kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya soka la Uholanzi. Hata hivyo, hakufani­kiwa kushinda taji lolote akiwa na klabu hiyo. Tatizo la mara kwa mara la goti lilisababisha atan­gaze kustaafu soka mwaka 2004 lakini alitengua uamuzi wake mwaka 2008 na kuelekea Go Ahead Eagle kwa msimu mmoja kabla ya kustaafu tena.

Overmars aliiichezea timu ya taifa ya Uholanzi kwa miaka 11. Alicheza mechi yake ya kwanza mwaka 1993 dhidi ya Uturuki na akatupia bao. Aliiwakilisha nchi hiyo katika michuano minne mikubwa; Kombe la Dunia 1994 na 1998 pamoja na Euro 2000 na 2004. Huko kote alishaini vilivyo, ingawa Uholanzi ili­kuwa bora lakini isiyokuwa na bahati ya mataji. Kwa ujumla alilichezea taifa lake mechi 86 na kufunga mabao 17 kuanzia 1993 hadi alipostaafu kuichezea timu hiyo mwaka 2004.

Kocha wake aliyemsajili Ajax, Van Gaal alimsifia Overmars kama mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga na kutoa pasi za mabao.

Overmars alikuwa win­ga aliyesifika kwa kutumia miguu yote miwili, kupiga chenga na kuwatoka ma­beki kwa ufundi mkubwa. Kasi yake ilisaba­bisha apewe majina mengi likiwemo la ‘Mfukuza Upepo’. Beki wa zamani, Gary Neville, amewahi kutamka kuwa Over­mars alikuwa winga bora zaidi ya wote aliowahi kukutana nao katika muda wote aliokuwa Manchester United, siyo tu kwa kuwa alikuwa ana uwezo wa kucheza upande wowote wa wingi na kuwachanganya wap­inzani kwa kuwa alikuwa hasomeki, bali pia kwa ufundi mwingi aliokuwa nao.

Katika kikosi cha Arsenal msimu wa 1997- 98, Overmars alikosolewa mno mwanzoni, hasa baada ya Arsenal kuambulia kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Blackburn Rovers na kushuka hadi nafasi ya tano kwenye msimamo. Lakini Wenger alisisitiza al­isajili mchezaji mzuri na lilikuwa ni su­ala la kupewa muda tu. Kweli kuanzia mwaka mpya, alibadilika na kuwa mtu hatari mno.

Wakati Arsenal ilipokutana na vinara Manchester United Machi 1998, Overmars alikuwa msumbufu mno kwao na katika dakika ya 80 al­ipokea mpira kutoka kwa Nicolas Anel­ka na kukimbia nao kwa kasi kabla ya kumtungua kipa Peter Schmeichel kwa ufundi. Arsenal ilishinda mechi hiyo na kubakiza pointi sita kabla ya kuifi­kia United, ikiwa na michezo mitatu mkononi.

Arsenal iliipiku Man U Aprili na kutwaa ubingwa kwa kuifunga Ever­ton Mei 3, 1998 katika mechi ambayo Overmars alifunga mabao mawili. Baa­daye wakatwaa ubingwa wa FA huku Overmars akifunga tena katika fainali. Msimu uliofuata, Overmars aliitesa tena Man United kwa kuifunga bao wakati waliposhinda 3-0 kwenye Ngao ya Jamii. Alifanya mengi mno.

MAFANIKIO YA SOKA

Alichokivuna wakati wote akicheza soka ni hiki:

Ajax:

Eredivisie: 1993–94, 1994–95, 1995– 96, KNVB Cup: 1992–93, Ngao ya Johan Cruijff: 1993, Ligi ya Mabingwa: 1994– 95, European Super Cup: 1995 na Inter­continental Cup: 1995.

Arsenal:

P r e ­m i e r : 1997–98, FA Cup: 1997– 98, Ngao ya Jamii: 1998.

TUZO BINAFSI:

Kipaji Bora cha Mwaka Uholanzi: 1992, Kiatu cha Dhahabu Uholanzi: 1993, Kinda Bora Zaidi Kombe la Dunia: 1994, Mchezaji Bora wa Mwaka Ajax: 1996.

MAISHA BINAFSI

Overmars alikulia katika masham­ba ya familia huko kwao Emst, katika Jimbo la Gelderland, Uholanzi. Na kila mwaka alikuwa akiwasaidia wazazi wake kuvuna viazi. Hawakuwa na mashine wala matrekta, hivyo walivu­na kwa mkono. Hata hivyo, baba yake alikuwa akimuita mtoto asiyetulia kwa kuwa akitoka shambani kazi yake ili­kuwa ni kucheza mpira tu. Overmars alimuoa mpenzi wake wa muda mrefu, Chantal van Woensel Mei 2013. Kabla ya ndoa hiyo walikuwa tayari na wa­toto wawili: Frenkie na Nick, wote sasa ni wanasoka.

ANACHOKIFANYA KWA SASA

Licha ya kwamba Overmars ni Mku­rugenzi wa Soka wa Ajax tangu 2012, ana biashara kibao. Ana hisa katika klabu yake ya zamani ya Go Ahead Ea­gles. Ni mmiliki mwenza wa mgahawa huko Epe anakoishi kwa sasa. Ana ma­jumba kadhaa amepangisha. Yeye na baba yake wanamiliki gereji. Ni tajiri. Mwaka 2002 alitokeza katika orodha ya matajiri 500 wa Uholanzi kwa mara ya kwanza.

Comments are closed.