The House of Favourite Newspapers

Oya masela Valentine hiyooo… meli ya sumu haina bandari!

0

Wakuu inaku-waje? Naamni ni mpango mzima na mishe zinasonga ileile. Naona pipo wanahaso si kitoto dheni tajeti hapa ni mkono uende kinywaji na mabovu yawepo mifukoni. Ama nene masela wangu. Ebana kila kichwa kisambaze lavu kwa mai namba wani wake si unanyaka tupo kwenye msimu wa kushoo lavu? Ndo kama hivyo mtu mzima nimeshatimba kwa fasi ya jamvini hapa unaonaje twende sambamba? Kaa humu wewe upate maudambwidambwi chaliiangu.

Washkaji zangu pamoko na ishu nyingine za kumeki laifu bati ishu ya kushoo lavu kwa wana na kupotezea michongo ya mizinguo fekelo.

Sasa bana mtu fedenge nakatiza kitaa kwa wana kujua kuna michongo gani inahapeni. Huku na huku napigwa na kitu cha sapraizi. Kucheki namiiti na bonge la shori chaliiangu ana stori lake moko anataka maushauri si unajua tena mi ndo kaka mkubwa?

Mkidi mkare hatare pale kati akaniminya kuwa yupo kwenye mastresi aibu. Nikaona isiwe kitu, nikamseti freshi akaanza kunimwagia maubuyu yake nene na nene. Aisee uspimie.

Shori ananiteli kuwa miezi bee iliyokrosi alikuwa na msela’ke ambaye alipanga kuwa naye foreva bati mwana akamzingua. Basi bana katika kuzinguana sistaduu akaona isiwe kitu bora akae pembeni kozi wanangu hii siyo taimu ya kuwa beneti na mwana ambaye ni marioo. Enzi hizo za kiloko zilishapita. Hii ni taimu ya kushea aidia ili laifu lisonge. Sasa inakuwaje eti msela kabisa anategemea alelewe na shori bila kupiga mingo za mahela si ni kutafutana ubaya huku?

Basi bana, baada ya mtoto mzuri kuzinguana na mwana akaanza kufaiti kusaka bingo si ndo akamingo na kachaa anayefaiti fyucha?

Baada ya msela marioo kunyaka mchongo si ndo akaanza kuleta za kuleta? Unaambiwa anadistabu kinoma hadi naiti kali shori halali inabidi amzimie kitu cha foni.

Mkidi kaapa kumwekea ngumu marioo kozi ameshaamua kula kona na kachala mwenye fyucha. Anakuteli kuwa meli ya sumu huwa haina bandari so yeye akishaona mwana anazingua huwa anamuona kama meli ya sumu so haweza kumpa tena kitu cha bandari ya moyo wake.

Unaambiwa Mario sasa hivi kaibuka na gia mpya baada ya kukutana na shori na msela wake kisha kupiga cha mbavu laivu na kuachwa mikono kichwani. Eti anamwambia arudishe majeshi la sivyo atamwekea patroo siku ya kitu cha Valentine’s Day ili amuharibie.

Basi bana mtoto mkare pale kati ameapa kutofanya mbwembwe na jamaa yake bati analaumu kinoma kuwa yule marioo kamkata kabisa stimu.

Wana mmenisoma? Acheni mizinguo mnapopewa chansi masti muwe makini msipoteze mingo za laifu hivihivi.

 

Kama vepe sii yuu

neksti wiki.

Leave A Reply