The House of Favourite Newspapers

NIMEKUWEKEA VICHEKESHO ‘VINAVYOPENDWA’ MTAANI KWETU

0
NIMEKUWEKEA VICHEKESHO 'VINAVYOPENDWA' MTAANI KWETU
Kicheko
  1. Huku mtaani maisha magumu mpaka jamaa ananiuliza: “Hivi luku haina kifurushi cha chuo?”

 

  1. Mlevi kakutwa akikojoa eneo la shule, Mwalimu Mkuu akamuuliza, hilo bango hapo limeandikwaje?

Mlevi akajibu: “USIKOJOE HAPA.”

Mwalimu: Kwa hiyo unafanya nini hapo?

Mlevi kwa umakini na upole akajibu: “HAKI YA MUNGU NILIJUA NDIYO JINA LA SHULE!”

 

  1. Ushawahi kukutana na demu anakwambia anasomaga chuo halafu anakutumia text inasomeka hivi:

“Za hasubui Lichadi, Humehamkaje, nirikuwa nakusalimiha tu hafya vipi?”

 

  1. Mwenye kiberiti anisaidie nataka niwashe data.

 

  1. Kuna jamaa anazunguka mtaani anatafuta watu 17 wa kuangalia naye muvi… Eti kwa sababu hiyo muvi imeandikwa 18 and above. Kingereza siyo Kizaramo, nae hapendagi ujingaa.

 

  1. Teacher: The president of Kenya is Kenyatta, who is the president of Ghana?

Student: Ghanatta.

 

  1. NIMEKUA single mpaka natamani kumuuliza mama wale waliokua wananiita mchumba wakati nipo mdogo wapo wapi?

 

  1. Hivi mama yenu yupo kama mama yangu? Akipika UGALI mchana usipokula ukabaki halafu jioni akipika WALI hakupi, mpaka ule UGALI wako uliobakizwa mchana. Ila akipika wali mchana usipokula Jioni akipika ugali Ukiuliza wali wako wa mchana anakwambia ulikuwa wapi wakati wenziyo wanakula?

 

UNAWEZA UKAONGEZA VYAKO PIA…

 

 

Leave A Reply