The House of Favourite Newspapers

Pablo: Hatutoki Kileleni Shirikisho

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Mhispania, Pablo Franco, amesema malengo yake ni kuhakikisha timu hiyo haishuki kileleni na kumaliza vinara wa Kundi D katika Kombe la Shirikisho Afrika, ili wajihakikishie nafasi ya kufanya vizuri zaidi hatua ya robo fainali.

 

Simba ikiwa inaongoza Kundi D ikikusanya alama saba, ikimaliza kinara kuna uwezekano mkubwa wa kutokutana na timu vigogo kama Pyramids, Orlando Pirates na Al Masry, zinazoongoza makundi yao.

 

Akizungumzia ishu hiyo, Pablo alifunguka kwamba: “Malengo yetu kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu ni kucheza angalau nusu fainali.

 

“Katika kufanikisha hilo, tunapaswa kufanya kazi kubwa michezo miwili ya mwisho ili kupata matokeo yatakayotuvusha.

“Tunataka kumaliza vinara wa kundi hili, ambapo hiyo itatusaidia kwa kiasi kikubwa kuwa na bahati ya kuanzia ugenini na kumalizia nyumbani hatua ya robo fainali.”

 

Simba itashuka dimbani Machi 20 mwaka huu ugenini kuwavaa ASEC Mimosas, kabla ya kumalizana na US Gendarmerie, Aprili 3, mwaka huu, Dimba la Mkapa, Dar.

Leave A Reply