The House of Favourite Newspapers

Pacha wa Saido Kutua Yanga, Amekipiga Ufaransa

0

YANGA wapo siriaz sana katika usajili huu wa dirisha dogo huku malengo yao makubwa yakiwa ni mwisho wa msimu huu kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara.

 

Hiyo ni baada ya kuingia kwenye rada za kumshusha straika wa zamani wa Angers ya Ufaransa, Fereboy Dore raia wa Congo ambaye anatajwa kama pacha wa Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’.

 

Yanga wanamtaka Dore mwenye umri wa miaka 31, ambaye alizaliwa katika Jiji la Brazzaville, Congo kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji la timu hiyo ambalo msimu huu lilianza kwa kusuasua.Inaelezwa kwamba, Yanga wanaweza kumpata kirahisi straika huyo kwani kwa sasa hana timu baada ya kuachana na Botev Plovdiv ya Bulgaria tangu Julai 2019.

Chanzo chetu makini kimeeleza kuwa, Yanga imepewa mchongo huo na kocha wao mkuu, Cedric Kaze akishirikiana na Saido. “Kuna dili la straika raia wa Congo, kama litatiki basi timu yetu itakuwa na uhakika wa kupata mabao mengi sana msimu huu.“

 

Huyo jamaa anaiwa Fereboy Dore, amewahi kucheza Ufaransa katika kikosi cha Angers, ni mpachika mabao mzuri sana.

 

“Kwa hili ngoja nimpongeze sana kocha wetu Kaze kwani ana jicho la mbali sana, amekuwa akituelekeza kutafuta wachezaji wa kigeni wenye historia nzuri kisoka, hivyo kama huyu jamaa atakubali kushuka kwenye hili dirisha dogo, basi ni uhakika kuwa kuna timu zitaoga mabao hadi 10,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Hivi karibuni, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Injinia Hersi Said, alijigamba kuwa wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na mchezaji ambaye atakuja kuingia moja kwa moja kikosini kama ilivyo kwa Saido ambapo wawili hao walikutana Ufaransa kati ya mwaka 2015 hadi 2016 ambapo Saido alikuwa akiitumikia Caen na Dore akiwa Angers.

 

Jamaa huyo alianzia soka lake kwao Congo akiichezea AS Kondzo katika msimu wa 2008‒2009, kisha akatimkia Ufaransa kwenye kikosi cha Angers akicheza hapo 2009 hadi 2013.

 

Akaenda Petrolul Ploiesti ya Romania, kisha Botev Plovdiv (Romania) ambapo akatolewa kwa mkopo kwenda CFR Cluj (Romania) akarejea Angers, akatua Clermont (Ufaransa) kwa mkopo kabla ya kutimkia tena Botev Plovdiv

 

STORI: MUSA MATEJA NA SAID ALLY, Dar es Salaam

Leave A Reply