The House of Favourite Newspapers

Pacome Ashusha Presha Yanga, Aitaka Robo Fainali CAF

0

KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua, ameshusha presha ndani ya kikosi hicho baada ya awali kupata majeraha ya bega, lakini sasa yupo fiti, huku mwenyewe akiahidi kuipambania timu hiyo katika michezo iliyosalia ya Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi D.

Wikiendi iliyopita, Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Al Ahly katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar, ambapo Pacome alifunga bao pekee la Yanga akisawazisha baada ya Percy Tau kuiweka mbele Al Ahly.

Katika mchezo huo, licha ya Pacome kumaliza dakika zote tisini, lakini alipata maumivu ya bega, akapatiwa matibabu na sasa yupo fiti kuivaa Medeama, Ijumaa ya wiki hii.

Akizungumza na Spoti Xtra, Pacome alisema anauchukulia kwa umuhimu mkubwa mchezo ujao ugenini dhidi ya Medeama watakaocheza huko Ghana, akiamini ushindi ndio utakaowarejeshea matumaini ya timu hiyo kufuzu hatua inayofuatia ya robo fainali.

Pacome alisema wamepanga kushinda michezo yote iliyobaki, kwa kuanza dhidi ya Medeama, licha ya ugumu wa mchezo huo, kwao wachezaji wamekubaliana kila mmoja kucheza kwa kujituma ili wafanikishe malengo yao.

“Tunakibarua kigumu cha kuhakikisha tunafuzu hatua inayofuatia ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kama yalivyokuwa malengo yetu msimu huu.

“Kwangu binafsi nitahakikisha ninaipambania timu yangu, katika michezo iliyopo mbele yetu kuhakikisha tunapata pointi tisa ambazo ninaamini zitatupeleka robo fainali.

“Ninataka kuona ninacheza katika kiwango bora katika michezo hiyo, kwa kuanzia huu uliokuwepo mbele yetu dhidi ya Medeama ambao watakuwepo nyumbani kwao, lakini hiyo haituzuii sisi kufanikisha malengo yetu ya ushindi,” alisema Pacome.

Yanga imesaliwa na mechi nne za hatua ya makundi, dhidi ya Medeama (ugenini na nyumbani), kisha CR Belouizdad (nyumbani), watamaliza na Al Ahly ugenini.

Kwa sasa Yanga ina pointi moja, inashika nafasi ya mwisho katika Kundi D. Al Ahly wanaongoza wakiwa na pointi nne, Medeama na CR Belouizdad, zote zina pointi tatu.

STORI NA WILBERT MOLANDI

KUTOKA GHANA: ALI KAMWE AFUNGUKA KABLA ya KUIVAA MEDEAMA – “MKIMPIGA AHMED ALLY MTAMUUA”…

Leave A Reply