The House of Favourite Newspapers

Padre wa Kanisa Katoliki nchini Marekani afariki baada ya kushambuliwa kanisani

0

Padre mmoja wa kanisa katoliki amefariki baada ya kushambuliwa katika eneo la kanisa katika jimbo la Nebraska nchini Marekani.

Polisi walisema walimpata Mchungaji Stephen Gutgsell na anayedaiwa kumshambulia kanisani baada ya kujibu simu ya 911 mapema Jumapili asubuhi katika jamii ndogo ya mjini Fort Calhoun.

Padre huyo mwenye umri wa miaka 65 alifariki kutokana na majeraha akiwa katika hospitali moja huko Omaha kufuatia shambulio hilo.

Mshukiwa aliwekwa chini ya ulinzi kanisani, polisi walisema. Baadaye walimtaja kwa jina Kierre Williams, 43, wa Sioux City, Iowa.

Alikamatwa kwa tuhuma za mauaji na matumizi ya silaha kufanya uhalifu, waliongeza.

Mchungaji Gutgsell aligonga vichwa vya habari mwaka wa 2007 baada ya kukiri kosa la kuiba $127,000 kutoka kwa parokia nyingine.

Alihukumiwa kifungo, akaamriwa kulipa pesa hizo na baadaye akatumwa tena katika kanisa tofauti.

Maafisa wa kanisa walisema wakati huo kwamba Kasisi Gutgsell alikuwa amejifunza.

Naye afisa polisi wa Kaunti ya Washington Mike Robinson, ambaye anachunguza shambulio hilo, alisema polisi hawakuamini kifo chake kinahusiana na kisa hicho.

UTATA! ‘KONEKSHENI’ za MASTAA ZINAZOVUJA MITANDAONI – KUNA UMUHIMU wa KUREKODI? | KONA ya MTAA…

Leave A Reply