The House of Favourite Newspapers

Pam D alia na Chid Benz

0

PAM-D-1.jpg

Pamela Daffa ‘Pam D

Na Mayasa Mariwata

MKALI wa Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ amesema kuwa, hali aliyonayo Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ kwa sasa kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya imekuwa ikimnyima usingizi kwa kuwa ni moja ya wasanii aliokuwa anawakubali.

Akibonga machache na Showbiz, Pam D anayebamba na Ngoma Ya Popolipopo alisema, wasanii wengi wanaingia kwenye mkumbo huo kutokana na kutotaka kupitwa na starehe za ujana pamoja na kuiga mambo ya wasanii wa nje matokeo yake wanaambulia maumivu, kama ilivyo kwa Chid na wengineo.Chidi-2

Rashid Makwiro ‘Chid Benz’

“Huwezi amini kuna muda huwa nakaa nikiangalia picha za Chid za kipindi cha nyuma na huyu wa sasa najikuta machozi yakinitoka kuona kipaji kama kile kinapotea bila sababu za msingi, kikubwa namuombea kwa Mungu aweze kuachana na hayo mambo kabisa japo najua kuna ugumu,” alisema Pam D.

Kwa sasa Chid yupo katika Kituo cha Life & Hope Rehabilitation Organization (Soba House) kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani akipatiwa huduma ya kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya ambapo hali yake inaendelea vizuri.

Leave A Reply