The House of Favourite Newspapers

Shoga; usipopika kwa wakati mumeo atakusaliti!

0

Ni Jumanne nyingine ambayo Mwenyezi Mungu ametujalia afya njema hivyo kila mmoja wetu amshukuru kwa jambo hilo la upendo.

Leo shoga yangu nitazungumza na wewe kuhusu ishu ya kuwahi kupika ambayo kuna baadhi ya wenzetu hawajui kama ni moja ya sababu za wanaume kutafuta michepuko.
Unaweza kukuta mama yupo makini katika usafi, tabia, upendo lakini akawa mzembe wa kupika kwa wakati na kuwa kero kwa mumewe.

Shoga, hakuna kitu ambacho wanaume hawakipendi kama wakifika nyumbani baada ya kazi na kukuta chakula hakijawa tayari.

Zaidi hukerwa na tabia hiyo kama ndani kunakuwa na kila kitu lakini matokeo yao licha ya kufika mapema wanakuja kuandaliwa chakula saa mbili, tatu au zaidi kisa mama kachelewa kupika.

Wanapowauliza wake zao sababu za kuchelewa kupika hawapewi jibu la kueleweka, sana sana mama atajitetea kwamba alikuwa anafua na kazi zingine.

Shoga; labda kama wewe ni mfanyakazi ukitoa utetezi huo kidogo anaweza kukuelewa lakini akina mama ninaowazungumzia hapa ni wale ambao hawafanyi kazi yaani mama wa nyumbani.

Kwa wewe mama ambaye tabia ya kuchelewa kupika ni sehemu ya maisha yako hivi mumeo akimtafuta kimada atakayekuwa akimjali na kumpikia kwa wakati utamlaumu?
Hebu basi kuwa makini katika jambo hilo kwani unapochelewa kupika utawalaza watoto wako na njaa kwani tabia ya watoto ikifika saa moja na nusuĀ  huhitaji kulala hivyo kushindwa kusubiri hiyo saa tatu unayomaliza kupika na kumkera mumeo ambaye kanunua kila kitu.

Leave A Reply