The House of Favourite Newspapers

Pam D, Lulu Diva wanaswa wakidendeka ‘live’

0

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ na muuza nyago maarufu, Lulu Abbasi ‘Lulu la Diva’ wamefumwa ‘live’ wakidendeka bila kujali macho ya watu, wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama jijini Dar.

Awali Lulu alikuwa ameketi siti ya jirani na Pam D huku kila mmoja akipiga maji kivyake, baada ya muda ndipo video queen huyo alihama na kumfuata bishosti  wakionekana na bashasha tele na kufikia hatua hiyo.

Lulu Diva alipoulizwa alisema; “Jamani wewe unanitafutia mabalaa mengine mbona sijafanya baya lolote zaidi ya kumhag kawaida na kumbusu kawaida tu isitoshe ndo nimeonana naye kwa mara ya kwanza,” alisema.

Kwa upande wake Pam D alisema Lulu alikuwa  MC wake siku hiyo hivyo ilikuwa lazima amchangamkie na hawakudendeka.

Leave A Reply