The House of Favourite Newspapers

Pam D nusura avuliwe gwanda na mjeda

0

pamdStori: Mwandishi wetu

Mwanadada anayefanya poa kwa sasa kwenye ulimwengu wa muziki, Pamella Daffa ‘Pam D’ ameelezea tukio lililompata hivi karibuni la kukumbana na mjeda aliyetaka kumvua suruali ya kijeshi aliyokuwa amevaa.

Akipiga stori na na paparazi wetu, Pam D alisema kuwa, siku hiyo alikuwa akitokea kwenye mishemishe zake, alipofika maeneo ya Magomeni alikutana na mwanajeshi ‘mjeda’ ambaye alimsimamisha na kumuuliza wapi amepata nguo hiyo.

 “Aliponisimamisha nilijua ni kwa sababu ya ile suruali, basi nikamwambia nimenunua, akaniambia eti nivue nimpe. Kwa kuwa alikuwa siriasi ilibidi nimbembeleze na ndipo akaniambia ananiachia ila siku nyingine nisiivae tena. Mh! Atanionea wapi?” alisema Pam D.

Leave A Reply