The House of Favourite Newspapers

Msiwazushie! Beyonce, Jay Z penzi spidi 120

0

beyonce-jay-z.jpgHawaii,  Marekani

Yamekuwa yakizuka madai kuwa mastaa wanandoa, Beyonce Knowles na mumewe Shawn Corey Carter ‘Jay Z’ wanafikiria kuachana ila ukweli ni kwamba mapenzi hayapungui na sasa mahaba yao spidi ni 120.

Kuonesha hivyo mara nyingi hutenga muda maalumu kwa ajili ya kwenda ufukweni kustarehe na kukarabati penzi lao ambalo mara nyingi watu huwatangazia kugombana na kutaka kupeana talaka.

Beyonce-Jay-Z-Best-PDA-Moments-Pictures.jpgHata hivyo, wawili hao juzikati walionekana tena kwenye fukwe za Hawaii ambako walienda kupunga upepo huku Beyonce akimuonesha mahaba mume wake sambamba na kutumia muda huo kupanga mambo makubwa.

Mambo waliyopanga huko ni pamoja na kuongeza nyumba nyingine jijini Los Angeles ambayo itagharimu dola milioni 93.

Mastaa hawa waliojaaliwa mtoto mmoja aitwaye Blue Ivy, kwao hata skendo ni pesa hivyo kuandikwa kuwa wana ugomvi mara kwa mara imekuwa haiwashtui kwani mambo yao yanaendelea kuwanyookea.

Leave A Reply