The House of Favourite Newspapers

PAPA GREGORY WA 13: Mwasisi wa Kalenda ya Sasa ‘Iliwapunja’ Watu Siku 13 Maishani!

0

HEBU tazama tarehe ya leo kwenye simu yako. Hebu tazama kalenda yako ukutani au popote il­ipo. Muulize mtu aliye karibu nawe leo ni tarehe ngapi. ‘Utagundua’ kwamba leo ni tarehe 1 Julai, 2017! Pamoja na imani yako ya kidini na kalenda zake, utaitambua kwanza tarehe hiyo.

Lakini umewahi kujiuliza nani aliyepanga kalenda unayoifuata na kuiamini hadi leo? Ni Papa Gre­gory wa 13 wa Kanisa Katoliki. Kalenda hiyo ndiyo inafuatwa karibu na watu wote duniani, bila kujali kalenda zao za kidini.

Kalenda ya sasa ni Kalenda ya Gregory, Waingereza wanaiita Gregorian Calendar. Huyu alikuwa ni Papa aliyezaliwa Januari 7, 1502 akafariki Aprili 10, 1585.

 

Alizaliwa akiitwa Ugo Boncompagni, baadaye akawa Gregory wa 13, jina alilopewa na Kanisa Katoliki Mei 13, 1572 hadi kifo chake 1585. Ndiye aliyeasisi na kuipanga kalenda hiyo iliyopewa jina lake mwaka 1582, ikachukua miaka zaidi ya 300 kwa nchi zote duniani kuanza kuitumia.

Kalenda hiyo iliisahihisha Kalenda ya Julian aliyekuwa Jenerali Julius Caesar wa Urumi, kwa asilimia 0.002. Kalenda ya Julius, iliyokuwa inaitwa Julian Calendar, aliianzisha wakati wa enzi yake mwaka 45 Kabla ya Kristo, ikichukua nafasi ya Kalenda ya Urumi.

 

Mabadiliko ya kalenda hiyo yalitokana na kutoonyesha kisahihi muda ambao Dunia hulizunguka Jua kwa mwaka. Kal­enda ya Julian ili­kuwa na mwaka mmoja mrefu kila baada ya miaka minne, ki­wango ambacho hakikuwa sahihi ambapo Kalenda ya Gregory ili­ipanga kiusahihi miaka mirefu kila mwaka.

 

Hata hivyo, watu walioishi wakati huo waliandamana wakipinga kal­enda hiyo mpya kuzifuta siku 13, zilizopunguza pia umri wao! Katika kusahihi­sha, wataalam walianza kuondoa siku kumi, wakaondoa tena siku 11, baadaye siku 12 na hatimaye kiusa­hihi wakaondoa siku 13!

Hata hivyo, waliolalamika wakati huo leo hawapo tena, hivyo Kalenda ya Gregory inaendelea bila matatizo.

 

Mwandishi: Walusanga Ndaki +255 715 439853

Leave A Reply