The House of Favourite Newspapers

Papaa Msofe awamwagia minoti warembo

0

Papa msofe (3)Abubakari Msofe ‘Papaa Msofe’ akigawa noti kwa warembo.

Na Dustan Shekidele, RISASI MCHANGANYIKO

MOROGORO: Mfanyabiashara maarufu nchini, Abubakari Msofe maarufu kama Papaa Msofe, wiki iliyopita aliwamwagia warembo minoti wakati wa shindano la kumtafuta mlimbwende wa Mkoa wa Morogoro, lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Nashera.

Papa msofe (2)Katika shindano hilo, ambalo denti wa Chuo cha St Joseph, Neema Chagula aliibuka mshindi wa kwanza, Papaa Msofe alianza kuonesha makeke wakati wa shoo iliyofanywa na Snura, hasa pale ‘alipowachezesha Chura’, kiasi kilichomfanya kuinuka na kwenda kumtunza dola kadhaa ambazo idadi yake haikuweza kufahamika mara moja.

Mfanyabiashara huyo aliyekuwa mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo, alitoa kiasi kikubwa cha fedha pia kwa mshindi wa kwanza ambaye pia alikabidhiwa shilingi laki tatu kwa kuibuka kidedea.

Papa msofe (1)Mshindi wa pili wa shindano hilo ambaye aliondoka na kitita cha shilingi laki mbili alikuwa ni Fatuma Salum na wa tatu, ambaye pia alipata shilingi laki moja kama zawadi, alikuwa Abela Joan.

Papaa Msofe ni mfanyabiashara ambaye alikaa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja baada ya kudaiwa kuhusika na mauaji ya Onesphory Kituli kabla ya kuachiwa mwishoni mwa mwaka jana baada ya kufutiwa shtaka hilo na kubadilishiwa lingine ambalo ni la kughushi, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Leave A Reply