The House of Favourite Newspapers

Patcho: FM Academia haina mpinzani

0

????????????????????????????????????

Patcho Mwamba.

MUSA MATEJA

MWANAMUZIKI wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ambaye pia hufanya vizuri kwenye tasnia ya Bongo Movies, Patcho Mwamba ametamba kuwa katika bendi zote za muziki wa dansi nchini, bendi yenye muziki mzuri ni FM Academia pekee.

patcho_mwambaAkizungumza na mwandishi wetu, Desemba Mosi, Patcho alisema kumekuwa na hisia mbovu kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa bendi hiyo wakilinganisha uwezo wa bendi hiyo na bendi zingine wakati ukweli upo wazi, wao wana muziki mzuri kutokana na ubora wa vyombo vyao.

“Niwaambie tu wanaojaribu kutufananisha na bendi nyingine Bongo, sisi hatuna mpinzani.

Kama ikitokea leo mapambambano yanayozingatia ubora wa muziki na wanamuziki wenyewe, basi FM Academia hakuna mtu anayeweza kuishinda kwenye ubora wa muziki na uimbaji wake,” alisema Patcho.

Leave A Reply