The House of Favourite Newspapers

PATRICK KUAGWA: Wema, Shilole, Manara Watoa Neno – Video

KUFUATIA msiba wa mtoto wa Muna ‘Patrick’, baadhi ya mastaa wa Bongo Movies, Bongo Fleva na soka wakiwemo Shilole, Wema, Haji Manara, Masanja Mkandamizaji, Asha Baraka na Kulwa Kikumba ‘Dude’ walipata fursa ya kutoa salam za rambirambi katika wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam leo Jumamosi, Julai 7, 2018.

 

Akizungumza wakati wa kutoa salam hizo, Masanja amewataka waombolezaji na Watanzania wote kuacha kuwahukumu Muna na mumewe Peter Zacharia kwa mapungufu yao, badala yake wawatie moyo na kuwaombea ili warudi kwenye uelewano mzuri na kuimarisha mahisiano. Pia amewataka waache kushadidia mambo ya umbea yasiyo na manufaa kwao badala yake wafanye mambo yanayompendeza Mungu.

 

Akiwakilisha wasanii wa Bongo Fleva, Shilole amesema;

“Mimi ni mzazi kama wazazi wengine, Patrick ni mtoto wangu, ni rahisi kama hayajakufika lakini yakikufika hili jambo siyo jepesi, pole sana muna na mume wako kwa kuondokewa na mtoto wenu. Ukiona tukio kama hili jiulize huenda kesho ni wewe.”

 

Naye Haji Manara akizungumza kwa niaba ya wanamichezo, amesema anawaombea wafiwa kwa Mungu ili awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

 

Akiwakilisha wasanii wa Bongo Movies, Wema amesema;

“Muna pole sana, najua ulivyompenda Patrick, na mapenzi yako kwake ndiyo yametufanya hata sisi tuwe hapa leo, mimi huwa napenda sana watoto, najua hakuna mzazi anayependa kumzika mwanaye, ninaamini Mwenyezi Mungu atakupa nguvu wewe na baba Patrick.

 

“Ninaomba tuyaache ya mitandaoni, najua mtoto wenu atafurahi huko aliko akiona mnaupendo na hakuna mgawanyiko kama huu ambao tumekuwa tukiuona. Muna unajua nakupenda na nitaendelea kukupenda, yaliyopita si ndwele tugange yajayo,” alisema Wema.

VIDEO: WEMA AKIFUNGUKA

Comments are closed.