The House of Favourite Newspapers

Paula Kajala Awachana Wateja Wake “Hebu Kuweni Serious Nyie, Mnasikitisha…”

0
Mrembo maarufu nchini Tanzania, Paula Kajala.

PAULA Kajala; ni mrembo maarufu nchini Tanzania ambaye amewachana baadhi ya wateja wake wanaodai anauza nguo zake bei ghali katika duka lake alilofungua hivi karibuni.

 

Baadhi ya wateja wanalalamika kwamba, kwenye duka hilo nguo ya bei ya chini ni shilingi elfu sabini na tano huku miwani akiuza shilingi elfu hamsini.

 

Hata hivyo, baada ya malalamiko hayo, Paula ameibuka na kuwachana wateja hao kwa kusema;

 

“Hebu kuweni serious nyie, yaani vitu vya Zara au H&M niwauzie elfu 20? Hamko serious, mnasikitisha…”

Paula alisema duka hilo limemgharimu shilingi milioni 500 za Kitanzania, jambo ambalo limepingwa na wengi.

UKWELI WOTE BARNABA KUSAINIWA WCB, KAJALA AMUONDOA HARMONIZE KITAMBI | HOTPOT

Leave A Reply