Penzi la Diamond Tanasha, Zengwe Jipya Laibuka!

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mwandani wake wa sasa, Tanasha Donna ‘Zara Zaire’

Zengwe kama lote! Habari ikufikie kuwa, lile penzi matata la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake wa sasa, Tanasha Donna ‘Zara Zaire’ limepigwa zengwe jipya, Risasi Mchanganyiko limedokezwa.

 

WAREJEA MITANDAONI

Wikiendi iliyopita wawili hao walirejesha mbwembwe za penzi lao kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukauka kwa wiki moja kwa kile walichodai wanataka mambo yao ya kimapenzi yawe ya binafsi zaidi.

 

 

ZENGWE LAIBUKA

Kufuatia kurejea huko kwenye mitandao ya kijamii na mahaba kama yote ndiko kukaibua zengwe kwamba, wawili hao walitengeneza penzi feki na walifanya hivyo ili kuipa kiki shoo yao ya Wasafi Festival iliyotarajiwa kufanyika leo kwenye Viwanja vya Mombasa Sports Club jijini Mombasa nchini Kenya.

Wakifanya yao.

WAKENYA SASA

Kwa mujibu wa baadhi ya Wakenya waliozungumzia mbwembwe hizo, penzi la Diamond au Mondi na Tanasha lina walakini kwani liliibuka kufuatia uwepo wa shoo hiyo iliyoandaliwa na Kituo cha Redio cha NRG anachofanyia kazi mrembo huyo akiwa ni mtangazaji wake.

 

“Hata hiyo kusema eti wameshindwa kuvumilia kuweka penzi lao ‘private’ na kuliondoa kwenye mitandao, ni gia ya kuamshaamsha baada ya kuona shoo imekaribia.

 

“Unajua penzi la Mondi na Tanasha liliibuka ghafla sana mara tu baada ya kuwepo kwa ratiba ya Tamasha la Wasafi hasa kwa upande wa Kenya ndiyo maana sisi tuna shaka.

 

“Pia ndiyo maana limekuwa na wakosoaji wengi hata Mombasa kwani wengi wanadai kuna kitu na siyo kupendana kwa dhati badala yake kuna biashara inaendelea kati yao.

“Wanasema hivyo kwa sababu hata redio iliyoandaa shoo hiyo ndiyo hiyohiyo anayofanyia kazi Tanasha na ni redio mpya inayohitaji kiki kwa hiyo tunaamini ni biashara ya kutafuta kiki ya shoo na redio.

“Watu wengi wanaamini Mondi na Tanasha wanawa-fool (kuwafanya wajinga) ili tu kutengeneza kiki ya hiyo shoo yao na wanaamini baada ya shoo ndiyo mwisho wa penzi hilo.

 

VIASHIRIA VINGI

“Kuna viashiria vingi kwamba mashabiki wanapigwa changa kwa sababu hata kwenye interview, Mondi alikuwa anahojiwa na redio moja jijini Mombasa akawa amesahau tarehe ya kufunga ndoa yao hivyo kuibua hisia kuwa hakuna ndoa hapo.

“Hii tu inatosha kuonesha hawa watu hawako serious,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Sisi yetu macho, lakini hatuoni dalili ya ndoa kati ya Mondi na Tanasha. Hatujaona muoaji na muolewaji kati ya Diamond na Tanasha.”

 

MPENZI WA ZAMANI AIBULIWA

Wakati hayo yakiendelea, mitandao mbalimbali ya Kenya wikiendi iliyopita ilimuibua aliyekuwa mpenzi wa Tanasha ambaye ni mwigizaji nchini Kenya aliyetajwa kwa jina la Nick Mutuma (pichani) ikieleza kuwa alishindwana na mrembo huyo kutokana na kupenda maisha ya starehe.

“Kwa muda mrefu alikuwa na Nick na waliachana tu mwaka jana mwishoni, hatukumuona na mwanaume mwingine hadi tulipomuona na Diamond, lakini ukweli ni kwamba alishindwana na Nick kwa sababu hakuwa na sifa za kuwa mke.

“Huwezi kumlinganisha na Zari (mzazi mwenza wa Mondi) hata kidogo. Zari ana sifa zote za mke,” kilisema chanzo kingine kutoka Mombasa, Kenya na kuongeza:

“Kwa Zari, Diamond alichezea shilingi chooni na hawezi kupata mke kama Zari.”

 

TANASHA ATETEA PENZI LAKE

Hata hivyo, akitetea penzi lake kwa Diamond baada ya kuwepo kwa wakosoaji kila kona, Tanasha alisambaza video wiki iliyopita akielezea kuwa, hajali maneno ya watu wenye chuki na anachojua Diamond anampenda na atamuoa.

“Bado ananitaka na ananipenda hivyo lazima atanioa,” alisema Tanasha.

Stori:SIFAEL PAUL, RISASI MCHANGANYIKO

Loading...

Toa comment