The House of Favourite Newspapers

Picha Ndiyo Kwanza linaanza Kwa Yanga Kesho

0

BAADA ya kuikosa michuano ya kimataifa kwa misimu miwili, Yanga wameibuka na kubainisha wazi kwamba kesho Jumapili ndiyo picha linaanza rasmi kwenye michuano hiyo.


Yanga kesho Jumapili
watashuka dimbani kuvaana na Rivers United ya nchini Nigeria katika mchezo wa hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Mchezo huo ambao unasubiriwa kwa hamu na Wanayanga kwa kutaka kuyaona majembe yao mapya yakianza kazi utapigwa saa kumi na moja kamili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

 

Katika mchezo huo, Yanga itawakosa wachezaji wake muhimu Mganda, Khalid Aucho na Wakongomani, Shaban Djuma na Fiston Mayele kutokana na vibali vyao (ITC) kuchelewa.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha Makipa wa Yanga, Razack Siwa amesema kuwa maandalizi na kikosi chao kipo fiti kuvaana dhidi ya Rivers.


Siwa alisema kuwa kikubwa
katika mchezo huo wanahitaji kupata ushindi mnono wa nyumbani kabla ya kurudiana Rivers huko Nigeria.

 

“Ushindi wa nyumbani ni kitu muhimu na lazima tuupate kuhakikisha tunatengeneza mazingira ya nyumbani kabla ya kurudiana dhidi ya Rivers kwao.“Wachezaji wapo katika morali ya juu kuhakikisha tunafanikisha malengo yetu ya kufika mbali katika michuano hii mikubwa ikiwemo fainali.

 

Katika mchezo huo tutawakosa wachezaji wetu watatu ambao ni Aucho, Djuma na Mayele ambao wamekosa ITC, lakini wao wachezaji wengine watakaochukua nafasi yao,” alisema Siwa.

Akizungumzia mchezo huo, mshambuliaji wa timu hiyo, Mkongomani Heritier Makambo alisema kuwa:

“Wanayanga wasubirie kupata
furaha kutoka kwetu, kwani maandalizi tuliyoyafanya yanatosha kupata matokeo mazuri katika mchezo huu.”


WANIGERIA WAKESHEA
VIDEO ZA MAKAMBO
Kwa upande wa Kocha wa
Rivers United, Stanley Eguma alisema kuwa “Kikosi changu
kipo fiti na tayari kuvaana na
Yanga kutokana na maandalizi niliyoyafanya.

 

“Nimeiona Yanga ni timu nzuri na nimewatahadharisha wachezaji wangu Makambo (Heritier) ndiye mchezaji tishio zaidi, nimewapa video zake kadhaa ikiwemo ya mchezo dhidi ya Zanaco.

 

“Katika video nilizoziona, nimepata picha nzima ya jinsi wanavyocheza na ni timu ya aina gani, wachezaji wa kuchungwa ni Makambo ambaye ni hatari.“Makambo yupo kwenye fomu nzuri ya ufungaji, ni mchezaji ambaye tunapaswa kuwa makini naye.

 

“Timu yangu kwa sasa inazifanyia kazi video zao kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sana na tunaweza kuwadhibiti tutakapokutana nao,” alisema Eguma.

WILBERT MOLANDI NA MARCO MZUMBE

Leave A Reply