Kartra

Arsenal Dimbani Leo na Rekodi Mbovu

WAKATI  ikishuka dimbani leo dhidi ya Norwich, Klabu ya Arsenal imeweka rekodi mbovu kwa mechi za mwanzo ndani ya Ligi Kuu England kwa kushindwa kukusanya pointi hata moja pamoja na bao.

 

Arsenal imecheza mechi tatu za Ligi Kuu England na haijafunga bao hata moja, rekodi inayowapasua kichwa washambuliaji na benchi la ufundi.

 

Rekodi nyingine mbovu, Arsenal ni ile ya kupiga shuti moja na halikuweza kulenga lango katika mechi zao tatu walizoshuka dimbani.

 

Ni rekodi mbovu ya Kocha Mkuu Mikel Arteta kwa kuwa amekuwa na ukuta nyanya, safu ya ushambuliaji inayoongozwa na nahodha Pierre Aubameyang ikiwa ni butu.

Arsenal inaburuza mkia itavaana na Norwich City ambayo ipo nafasi ya 19 kwenye msimamo EPL.


Toa comment