The House of Favourite Newspapers

Picha: Shuguli ya Mazishi ya Kitaifa ya Rais wa Zamani wa Kenya Emilio Mwai Kibaki

0
Mwili wa Rais wa zamani wa Kenya Emilio Mwai Kibaki katika hifadhi ya miili – Lee Funeral Home na kuupeleka Ikulu, Nairobi ambako mwili wake ulipokelewa na Rais Uhuru Kenyatta na Mke wa Rais Margaret Kenyatta kabla ya kusindikizwa na Mkuu huyo wa nchi katika Uwanja wa taifa wa Nyayo kwa ajili ya mazishi ya kitaifa

MAZISHI ya kitaifa yanafanyika leo Ijumaa kwa ajili Rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki aliyefariki wiki moja iliyopita akiwa na umri wa miaka 90.

 

Marais kadhaa wa Arika na viongozi wengine waheshimiwa wa dunia watashiriki, huku Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Salva Kiir wa Sudan Kusinina wa Ethiopia Sahle-Work Zewde wakiwa tayari wamethibitisha kuhudhuria mazishi hayo. Zifuatazo ni picha za matukio ya utaratibu wa mazishi ya kitaifa ya rais huyo wa zamani wa Kenya:

Rais wa Kenya uhuru Kenyatta na Mke wa Rais Margareth Kenyatta wakiwa tayari kuupokea mwili wa mtangulizi wake hayati Emilio Mwai Kibaki kabla ya kuusindikiza katika uwanja wa taifa wa Nyayo kwa ajii ya mazishi ya kitaifa.
Picha ya hayati Rais wa zamani wa Kenya Emilio Mwai Kibaki, ikiwa imesimamishwa kwenye Uwanja wa taifa wa Nyayo mjini Nairobi, ambako Wakenya na viongozi wa nchi na wa kimataifa wanafanya mazishi ya kitaifa kufuatia kifo chake kilichotokea wiki iliyopita.
Mwili wa hayati Mwai Kibaki ukisindikizwa mapema leo kuelekea Uwanja wa taifa wa Nyayo kwa ajili ya taratibu za mazishi ya kitaifa.
Baadhi ya Wakenya wakiwa katika Uwanja wa taifa wa Nyayo kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya kitaifa ya Rais wao wa zamani wao Emilio Mwai Kibaki.
Mwili wa hayati Rais wa zamani wa zamani wa Kenya Emilio Mwai Kibaki ukiingizwa ndani ya uwanja wa taifa wa Nyayo ukisindikizwa na Vikosi vya ulinzi vya Kenya. Mazishi ya kitaifa yanafanyika katika Uwanja wa Nyayo Ijumaa

Leave A Reply