The House of Favourite Newspapers

Wema Sepetu Ahamia CHADEMA

Kutoka kushoto ni Mama Wema, Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya pamoja na staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.

Wema na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wakiwa wameketi ndani ya Mahakama Kuu kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi ya kikatiba ya Mbowe leo.

Ester Bulaya akiteta na Mama Wema.

Ester Bulaya na Wema wakionesha vidole viwili ambayo ishara ya CHADEMA

Wema akionesha ishara ya CHADEMA mahakamani hapo.

STAA wa Bongo Movies, Wema Sepetu amedaiwa kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kuonekana akiwa bega kwa bega na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Wema na mama yake mzazi, Mariam Sepetu wameonekana mahakamani leo Februari 23, 2017 wakifuatilia kesi ya kikatiba ya Mbowe aliyoifungua dhidi ya RC Paul Makonda, Kamanda Simon Sirro na Kamanda Wambura baada ya kuhusishwa kwenye sakata la biashara ya madawa ya kulevya.

Wema alionekana mara kwa mara akinyanyua vidole viwili ambayo ni ishara ya salamu ya Chadema huku Mbunge Ester Bulaya akimsapoti ndani ya viunga vya mahakama hiyo.

Wema anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo yote yanahusisha matumizi ya dawa za kulevya (bangi) ambapo kesi yake inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Ksutu. Kesi hiyo iliahirishwa jana kutokana na upelelezi kutokamilika na itatajwa tena Machi 15, 2017.

Aidha, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilianio wa Chadema, Tumaini Makene amesema leo (Alhamisi) kuwa kupitia kwa Mwenyekiti wa Chama hico Taifa, Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza na Umma kupitia waandishi wa habari na kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo msanii Wema Sepetu.

Mbowe na Lissu wanawasilisha hati ya mashitaka iliyorekebishwa na kumuongeza Mwanasheria Mkuu.

Msanii huyo aliyeshinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, alikuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuhamia Chadema.

PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS
TAZAMA VIDEO HAPA

Comments are closed.