The House of Favourite Newspapers

Pigo PSG Neymar Nje Msimu Mzima kufanyiwa Upasuaji Doha, Qatar

0

MSHAMBULIAJI wa Paris St Germain, Neymar anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu huko Doha, Qatar na hii itamfanya akose mechi zote zilizosalia msimu huu.

Neymar, ambaye amefunga mabao 13 na asisti 11 katika Ligue 1 msimu huu hakucheza tangu alipoumia kwenye mchezo dhidi ya Lille Februari mwaka huu ambao PSG walishinda 4-3 na tangu hapo amekosa michezo miwili iliyopita.

Mshambuliaji huyo ataukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Bayern Munich leo Jumatano ukiwa ni wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mbaingwa Ulaya.

Hii sio mara ya kwanza kwa Mbrazil huyo kukosa mechi muhimu akiwa PSG kutokana na majeraha mbalimbali tangu ajiunge nao kwa dau la rekodi ya dola mil 269 mwaka 2017 akitokea Barcelona.

Aidha kwenye Kombe la Dunia lililofanyika mwishoni mwa maka jana, Neymar aliumia enka na alikosa mechi kadhaa kabla ya kurejea dimbani kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil.

Taarifa iliyotolewa na PSG ilisema kuwa, baada ya Neymar kuumia wafanyakazi wa kitengo cha udaktari cha timu hiyo walipendekeza upasuaji wa kurekebisha mishipa ili kuepusha hatari kubwa ya kujirudia kwa tatizo hilo.

Aidha iliongeza kuwa upasuaji huo utafanyika huko Doha nchini Qatar hivyo mchezaji huyo atakuwa nje kwa miezi mitatu hadi minne kabla ya kurejea na kuanza mazoezi.

Leave A Reply