The House of Favourite Newspapers

Pluijm Awapa Mbinu Kagere, Okwi

Hans Pluijm (kulia).

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Mholanzi Hans Pluijm amewataka nyota wa Simba ambao leo wataanza kwenye mchezo dhidi ya JS Saoura ya Algeria kutafuta matokeo haraka na kulinda pumzi ya kutosha.

 

Simba inakutana na Js Saoura katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Pluijm ambaye alifanikiwa kuifundisha Yanga na kuifikisha hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, amesema kikubwa ambacho wachezaji wa Simba wanatakiwa kukifanya ni kulinda pumzi yao iwe ya kutosha na kutafuta mabao ya mapema.

 

“Nipo Zanzibar kwa sasa nimepata bahati ya kuona kikosi cha Simba kikiwa uwanjani, wana wachezaji wazuri na bora hasa linapokuja suala la kutafuta matokeo, hivyo wanachotakiwa kuboresha ni kulinda pumzi yao isikate mapema na kutafuta ushindi wa mapema uwanjani.

 

“Wachezaji wao wengi wana uwezo na uzoefu na mechi za kimataifa, Kagere (Meddie), Okwi (Emmanuel), Chama (Clatous) na Wawa (Pascal) sasa hawa wasicheze wao wenyewe bali wacheze wakiwa ni timu hapo ndipo watapata matokeo ambayo wanayataka, hakuna haja ya kuwa na hofu kila kitu kinawezekana,” alisema Pluijm.

Stori na Lunyamadzo Mlyuka

Comments are closed.