The House of Favourite Newspapers

Pogba Ahofia Kukosa Kombe la Dunia Kama Akifanyiwa Oparesheni ya Goti

0
           KIUNGO wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Juventus, Paul Pogba

KIUNGO wa Juventus, Paul Pogba, ana hofu kuwa anaweza kukosa fainali za Kombe la Dunia kama atalazimika kufanyiwa oparesheni ya goti. Mfaransa huyo, hivi karibuni alionekana kuwa na majeraha ya goti la kulia kwenye pre-season huko Marekani.

 

Badala ya kufanyiwa upasuaji Marekani, Pogba alipaa kurudi Italia wiki iliyopita kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa majeraha hayo.

Na kwa mujibu wa Gazetta dello Sport, nyota huyo wa zamani wa Manchester United, kwa sasa anafikiria upi utakuwa ni uamizi sahihi zaidi kati ya oparesheni mbili ambazo mojawapo ni lazima aifanye. Pogba, 29, anatakiwa aondolewe baadhi ya chembechembe kwenye goti lake na kulazimika kukaa nje kwa siku 40 hadi 60.

 

Lakini athari zake ni kwamba anaweza asiwe fiti kwa asilimia 100 kwa kuwa oparesheni hiyo inawafaa wachezaji wadogo zaidi.

Oparesheni ya pili ambayo anaweza kufanya ni ile kubwa, ya kumaliza tatizo kabisa. Lakini itamweka nje ya uwanja kwa miezi mitano, ikimaanisha kuwa akifanya hiyo, atakosekana kwenye Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar

Leave A Reply