The House of Favourite Newspapers

Pogba, Man U Mwisho Wao Umefika

0

MAISHA ya Paul Pogba ndani ya Manchester United ni kama yamefika mwisho na sasa kilichobaki ni pande hizo mbili kukubaliana juu ya kuachana. Hatua hiyo inaenda mbele zaidi ambapo hata wachezaji wenzake kikosini hapo wanaamini kuwa itakuwa ngumu kwa mchezaji huyo kubadili mawazo yake kuendelea kuichezea United.

 

Pogba raia wa Ufaransa inadaiwa kuwa anaona timu yake bado ipo nyuma sana katika mbio za kutafuta mataji nyuma ya Manchester City na Liverpool, ndiyo maana anaona ni muda sahihi wa kuondoka klabuni hapo.

 

Hadi sasa Pogba, 26, amecheza mechi mbili tu tangu Septemba, akiwa anasumbuliwa na majeraha ya kifundo cha mguu, huku ikiaminika hata kocha wake, Ole Gunner Solskjaer naye ameshakata tamaa juu yake.

Klabu ya Real Madrid ipo tayari kumpokea Pogba lakini inaangalia uwezekano wa kumtoa Toni Kroos, 29, ambaye bado ana mkataba wa muda mrefu na timu hiyo. Inaelezwa kuwa kinachokwamisha uhamisho wa Pogba hadi sasa ni suala la ada yake ya usajili kwa kuwa Juventus nayo ipo tayari kumsajili.

Watu wa ndani wa United wanasema kuwa licha ya Solskjaer kujitokeza hadharani na kumuunga mkono mchezaji wake lakini nyuma ya pazia amevurugwa na kinachoendelea juu ya mchezaji huyo na yupo tayari kumru-husu aondoke. Wakati huohuo, imee-lezwa kuwa Pogba alicheza akiwa na maumivu katika mechi zake mbili alizorejea uwanjani hivi karibuni dhidi ya Watford na Newcastle, ndiyo maana akaumia tena na sasa anatakiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili.

Leave A Reply