The House of Favourite Newspapers

Polisi Amuua Rafiki Yake Wakitafuna Mirungi Kituoni

0

MAOFISA wa upelelezi kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini Kenya wameanzisha uchunguzi dhidi ya kifo cha raia aliyekuwa ametembelea Kituo cha Polisi cha Nyari, eneo la Gigiri, Nairobi.

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mkuu wa DCI George Kinoti, marehemu alikuwa amekwenda kumtembela rafiki yake katika kituo hicho aliyefahamika kwa jina la Konstebo Edgar Mokamba usiku wa Jumanne, Disemba 29.

 

Kinoti alisema kutokana na mkasa huo, Mokamba kwa sasa anashikiliwa kama mshukiwa wa mauaji ya swahiba wake.

Aidha, taarifa za awali zinaonesha kuwa wawili hao walikuwa wanajiburudisha kwa kutafuna mirungi kituoni humo ambapo Mokamba alikuwa anahudumu kama mlinzi wa zamu wakati mkasa huo ulipotokea.

 

“Milio ya risasi ilisikika saa chache baadaye ambapo ofisa aliyekuwa kwenye zamu alikimbia katika eneo la tukio na kukutana na maiti kwenye kiti cha dereva cha gari lake aina ya Toyota Probox.

 

“Ofisa huyo ambaye alikuwa anatafuna mirungi na marehemu alipokonywa silaha na kukamatwa baada ya kumpiga mwenzie risasi mara 10,” alisema.

Akiwa kwenye selo, makachero wameanzisha uchunguzi kubaini sababu za mauji hayo,” alisema DCI.

 

Kisa hiki kimekuja siku chache baada ya vyombo vya habari nchini humo kuripoti kuwa ofisa wa jeshi nchini humo, alishambuliwa na kupigwa hadi kufa na kundi la watu sita katika eneo la jengo la utawala jijini Nairobi.

 

Kwa mujibu wa DCI, ofisa huyo na kaka yake walijiburudisha kwa vinywaji siku ya Disemba 25, 2020 katika klabu moja na walikutana na wanandoa ambao ofisa huyo aliamua kumsalimia mwanamke.

 

Mume wa mwanamke huyo alikerwa na kitendo hicho na kutoleana maneno machafu kisha wakaanza kuruyshia mawe ambayo yalisababisha ofisa kupoteza maisha kutokana na majeraha.

STORI: MWANDISHI WETU NA MITANDAO

Leave A Reply