The House of Favourite Newspapers

Polisi Dar: Usalama wa Kutosha Sikukuu ya Idd

0

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema limeimarisha ulinzi kuelekea Sikukuu ya Eid El Fitr sambamba na kupiga marufuku disko toto kwenye kumbi mbalimbali za starehe.

 

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa jeshi hilo limejipanga kuimarisha doria katika maeneo yote muhimu zikiwemo nyumba za ibada, kumbi za sterehe na fukwe.

 

Pia Kamanda Mambosasa amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao hawatembei peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu na wasiwaruhusu kuogelea peke yao, akisema hatua hiyo itazuia vifo vya vinavyotoka na watu kuzama kwenye maji.

Leave A Reply