The House of Favourite Newspapers

Polisi: Dereva Aliyekamatwa, Akafa, Alikuwa na Homa ya Mapafu

0

 

JESHI la Polisi mkoani Mbeya limesema dereva wa lori, Abrahaman Hussein (61) aliyefariki dunia muda mfupi baada ya kumkamata alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa homa ya mapafu.

 

Hayo yameelezwa leo Jumamosi Januari 30, 2021 na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Jerome Ngowi, akibainisha kuwa Hussein akiwa njiani alijisikia vibaya na madereva wenzake walimpeleka hospitali ya Chimala na baada ya vipimo alikutwa na ugonjwa huo.

 

 

Video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha askari polisi takribani wanne wakiwa wamelizunguka lori hilo na mmoja akimvuta dereva huyo, ambaye ni mkazi wa Tunduma mkoani Songwe, Januari 28, 2021.

 

 

Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya polisi kukamata lori hilo, na kumtaka ashuke na alipofanikiwa, wote walimbeba na kumweka kando ya barabara huku dereva huyo akionekana kukosa nguvu.

 

Kutokana na tukio hilo, baadhi ya habari zilizosambaa mitandaoni zilidai kuwa dereva huyo alikamatwa na polisi na kupewa kichapo kikali ambapo inadaiwa alipelekwa kituo cha polisi ambako umauti ulimkuta lakini jeshi la polisi mkoani Mbeya limekanusha taarifa hizo.

Leave A Reply