The House of Favourite Newspapers

Polisi Waamua Kuhusu Chris Brown Akituhumiwa Kubaka

 

MWANAMUZIKI wa Marekani,  Christopher Maurice Brown maarufu kama Chris Brown,  ameachiwa huru na polisi bila dhamana jijini Paris, Ufaransa,  baada ya kukamatwa na kuhojiwa leo, Januari  23,  juu ya tuhuma za mwanamke wa Ufaransa aliyesema amembaka.

 

Baada ya kuachiwa msanii huyo alikanusha taarifa za mwanamke huyo kuhusiana na kumfanyia tukio hilo huku post hiyo ikiandamana na picha iliyokuwa na maandishi yaliyosomeka ‘This Bitch Lyin’.

 

“Nataka kuweka mambo sawa, huu ni uwongo, huku ni kunivunjia heshima kwa mwanangu na familia yangu kwa hadhi niliyonayo” aliandika Breezy kwenye akaunti yake ya instagram.

 

 

Mwanasheria wa Chris Brown amefunguka na kusema kwamba madai yaliyokuwa yanamkabili msanii huyo si ya kweli,  ni uongo mtupu.

 

Chris Brown anaruhusiwa kuondoka Ufaransa muda wowote kuanzia sasa kwa sababu hana kesi inayomkabili.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.