The House of Favourite Newspapers

Polisi Wakamata Magari 8 Tukio la Lissu, Wamsaka Dereva Wake

0
Dereva wa Lissu akizungumza na Mbowe.

KAMANDA wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amemtaka dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu, ajitokeze  ili aweze kutoa maelezo yake kuhusiana na tukio  la kupigwa risasi bosi wake.

Kamanda  huyo amesema kwamba sababu ya kumtafuta dereva huyo aliyemtaja kwa jina la Adam ni kwa sababu alikuwa pamoja na  majeruhi wakati tukio hilo linatokea.

Katibu Mkuu wa Chadema Dk Vicent Mashinji.

Pia Kamanda huyo alimtaka  Katibu Mkuu wa Chadema Dk Vicent  Mashinji kufika  kwa RCO mjini Dar es Salaam ama Dodoma  kutokana kauli yake kuwa katika uchunguzi wao wamewabaini wahusika.

Kamanda  Muroto amesema Polisi Mkoani Dodoma wamekamata magari nane aina ya Nissan Patrol kwa ajili ya uchunguzi wa tukio la kupigwa kwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu.

Kamanda Muroto amesema uchunguzi huo unafanywa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA).

“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa wahalifu walikuwa na silaha ya SMG/SAR kutokana na maganda  ya risasi yaliyokutwa eneo,” amesema

Leave A Reply