The House of Favourite Newspapers

Polisi wanzingira nyumba ya Gwajima

0

1 2 3 4Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaoongozwa na Askofu Josephat Gwajima wakiwa nje ya geti la kiongozi huyo.

gwajima2

Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajim.

POLISI wanaotajwa kuvaa nguo za kiraia (askari kanzu),  wanadaiwa kuzingira nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, Salasala nje kidogo ya jijini Dar es Salaam majira ya saa nane mchana.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vinadai kuwa askari hao walifika nyumbani kwa askofu huyo mchana huo ambapo ilielezwa kuwa baada ya kufika kwa kiongozi huyo wa kiroho waligonga geti lakini halikuweza kufunguliwa na kuamua kuweka kambi kwa muda wa saa mbili.

Ilielezwa kuwa mlinzi wa geti hilo hakuweza kufungua wala kutoka ndani hadi askari hao walipoondoka eneo hilo.

Mwandishi wa mtandao huu alifika eneo la tukio na hakukuta askari hao kwani walikuwa wameshaondoka japokuwa kulikuwa na waumuni wa kanisa hilo nje ya geti.

Hata hivyo walipoulizwa juu ya uwepo wa askari walisema hawajui lolote.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Christopher Fuime alipoulizwa na mwandishi wetu kuhusiana na madai hayo alikiri kuwa askari wake walikwenda kwa Gwajima.

“Askari wangu walikwenda kumuona Gwajima lakini hawakumkuta, hivyo wakarudi ofisini,” alisema kamanda Fuime bila kufafanua nia ya kumfuata kiongozi huyo wa kiroho.

Leave A Reply