The House of Favourite Newspapers

Polisi Yakamata Bunduki, Bangi, Nyara Za Serikali

0

1.Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai CP, Diwan Athuman, akitoa taarifa yake.

2.Wanahabri wakichukua matukio.Wanahabari wakichukua matukio.3.Akizidi kutoa ufafanuzi wa jambo.CP Athuman akifanua jambo.

4.Wanahabri wakisikiliza kwa makini.Wanahabari wakisikiliza kwa makini kilichokuwa kikiendelea kwenye hafla hiyo.

JESHI la polisi nchini kwa kushirikiana na ofisi za polisi wa kimataifa,  Interpol, kanda ya Kusini mwa Afrika  (Southern  Africa Regional Polisi Chief Co-operation – SARPCC0) zilizopo Harare  nchini Zimbabwe limefanikiwa kukamata bunduki, bangi  na nyaraka za serikali.

Akizungumza na wanahabari leo kwenye ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, CP Diwan Athuman amesema kuwa oparesheni hiyo iliyofanyika ilitokana na maamuzi yaliyofikiwa kwenye mikutano ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) baada ya kufanya kikao chao mwezi Mei mwaka huu nchini Afrika Kusini.

CP Athumani alizitaja silaha zilizokamatwa katika oparesheni hiyo kuwa ni SMG mbili, magobore  mawili, bastola mbili  na milipuko aina ya 42 EME  huku  wahamiaji haramu saba wakikamatwa kutoka  Kenya ambapo walikamatiwa Zanzinbar, wahamiaji kutoka Burundi walikamatiwa Mkoa wa Kigoma, na mhamiaji mmoja aliyekuwa ametokea nchi ya Zambia kukamatiwa Mkoa wa Ruvuma.

Aidha kamanda huyo alisema kuwa bidhaa bandia na dawa zilizopigwa marufuku zilikamatwa zikiwa na  thamani ya shilingi milioni 3.5 milioni  na mafuta ya kupikia aina ya Malo ya kilo 30 pia yalikamatwa..

Oparesheni hiyo iliyopewa jina la ‘Oparesheni Lephalale’ ilishirikiana na idara za taasisi za serikali za wanyama pori, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Ushuru wa Forodha (TRA)  zote zikiwa na lengo la kuongeza nguvu na tija kupamabana dhidi ya wahalifu.

Aidha alisema kuwa  katika oparesheni hiyo mikoa iligawanywa katika kanda nane yaani, kanda ya kaskazini, kanda ya nyanda za juu kusini, kanda ya Dar es Salaam, kanda ya ziwa, kanda ya magharibi, kanda ya Zanzibar, kanda ya kati na kanda ya kusini.

Kamanda alieleza mafaniko makubwa yaliyopatikana kutokana na oparesheni  kuwa ni pamoja na vielelezo na watuhumiwa mbalimbali wa makosa yaliyopewa kipaumbele na  ambayo hayakupewa kipaumbele, akisema kuwa jumla ya magari 756 yaliyoibiwa  yaligunduliwa, kati ya hayo magari mawili yaliibwa kutoka Afrika ya Kusini, ikiwa ni pamoja na pikipiki saba.

Vilevile alisema jeshi la polisi halitakubali kamwe kuona kundi la watu wachache linatishia usalama wa maisha na mali za raia wema, hivyo watakaobainika watakamatwa na hatimaye kuchukuliwa hatua za kisheria.

 NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply