The House of Favourite Newspapers

Polisi Yavamia Ukumbi, Yazuia Mkutano wa ACT – Wazalendo Dar

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limezuia mkutano wa ndani wa chama cha ACT-Wazalendo uliokuwa ufanyike leo, Jumatano, Machi 27, 2019 asubuhi katika ukumbi wa PR, Temeke jijini Dar es Salaam.

 

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema wameuzuia baada ya kufanya uchunguzi na kubaini viashiria vya kutokea vurugu katika mkutano huo na kusema kutokana na polisi kuwa na shughuli nyingine hawawezi kuimarisha ulinzi eneo hilo na kuwataka wahusika wasubiri mpaka hali itakapotulia.

 

“Mkutano wa ndani hauhitaji maombi ya kibali, ila shida kipindi hiki cha mpito hivi vyama vya ACT na CUF kumekuwa na uhasama wa chini kwa chini, tumepata taarifa watu wa CUF walikuwa wamejipanga kufanya vurugu pale. Kwa kuwa sisi hatukuwa na zuio, tukaona hatuna sababu ya kuacha watu wakavurugana na kuumizana. Kuna sintofahamu tukaona si kipindi sahihi za kuacha huu mkutano ufanyike kwa sasa,” amesema.

 

Kwa upande ake Katibu Mwnezi ACT, Ado Shaibu amesema kuwa polisi wamezuia mkutano huo baada ya kufika eneo la tukio na kuwataka viongozi na wanachama wa chama wote kutawanyika.

 

Viongozi waliotarajiwa kushiriki mkutano huo ni kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe, Maalim Seif Sharif Hamad, Naibu Kiongozi wa chama hicho, Duni Haji, mwenyekiti taifa, Yeremia Maganja, makamu mwenyekiti Bara, Shaaban Mambo, Katibu Mkuu, Dorothy Semu na naibu katibu mkuu, Msafiri Mtemelwa.

Wabunge Cuf Wawajia Juu Wanachama ACT

Comments are closed.