The House of Favourite Newspapers

PPF Waendelea Kuhakiki Wastaafu!

ppf-3Meneja Kiongozi Pensheni na Huduma za Wanachama PPF, John Mwalisu (katikati) akifafanua jambo.

ppf-2Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Janet Ezekiel (anayezungumza) na kushoto kwake ni Meneja Kiongozi Pensheni na Huduma za Wanachama, John Mwalisu na Meneja Uhusiano PPF, Lulu Mengele.

ppf-1Viongozi hao wakisikiliza maswali ya wanahabari (hawapo pichani) yaliyokuwa yakiulizwa.

ppf-4Baadhi ya wanahabari wakichukua tarifa hiyo.

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii wa PPF umewatarifu wanachama wake juu ya muendelezo wa  zoezi la kuhakiki wastaafu wanalolifanya kila baada ya miaka miwili ili kuwa na kumbukumbu sahihi za wastaafu wao ambao wanawalipa pensheni kila mwezi.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), Meneja Kiongozi wa Huduma za Pensheni  PPF, John Mwalisu amesema zoezi hilo limekwisha anza tangu Septemba 12, mwaka huu na limekamilika leo kwenye mikoa mitatu ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Zanzibar.

Mwalisu amesema wamekuwa zoezi hilo ni endelevu hivyo kwa wale wasiopata nafasi hiyo wasitie shaka kwani watahakikiwa kama kawaida.

“Lengo letu ni kuweka kumbukumbu sahihi za wastaafu tunaowalipa kila mwezi maana hili ni daftari na kuna watu wamebadili maeneo wanayoishi ama sehemu ya kuchukulia fedha hivyo tunafanya hivi ili kuoanisha taarifa zao ili tusije kumpa mtu malipo yasiyostahili,”alisema Mwalisu.

Aidha, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Janet Ezekiel ameitaja mikoa mingine ambayo zoezi hilo linatarajiwa kuhakikiwa kuwa ni Morogoro, Singida na Dodoma (Septemba 26 hadi 30, mwaka huu), Mwanza, Mara na Kagera (Oktoba 3 hadi 7, mwaka hu), Mbeya, Iringa na Rukwa (Oktoba 17 hadi 21, mwaka huu) na Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Mtwara (Oktoba 24 had 28, mwaka huu).

Na Denis Mtima/GPL.

Comments are closed.