The House of Favourite Newspapers

Profesa Jay na Sababu za Kuacha Muziki

Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay,

WANAMUZIKI ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay, amefunguka kuwa hataacha muziki kamwe, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwasaliti wananchi wake ambao wamemfahamu na kumpeleka mjengoni kupitia muziki wake alioufanya kwa miaka mingi.

 

Professor Jay ambaye anajiita mbunge wa binadamu na wanyama kutokana na Hifadhi ya Mbuga ya Mikumi kuwa kwenye jimbo lake, alisema hayo hivi karibuni alipokuwa akitambulisha wimbo wake mpya uitwao Pagamisa ambao amemshirikisha Prodyuza Mr. T Touch.

 

Prodyuza Mr. T Touch.

“Pagamisa ni kazi nzuri ambayo imepokelewa vizuri na kiukweli miaka yote ya maisha yangu nitaendelea kutoa kazi nzuri na siwezi kamwe kuacha muziki kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwasaliti wananchi ambao wamenipeleka mjengoni kupitia muziki huu ambao ninafanya,” alisema Professor Jay.

STORI: BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.