The House of Favourite Newspapers

Pumzika kwa amani daudi zabron!

0

Na Musa Mateja

MAJONZI! Mdogo wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers, Eric James Shigongo aitwaye Daudi Zabron, juzikati aliingiza kwenye majonzi familia ya mzee Zabron Bukumbi wa kijijini Bupandwamhela, Sengerema mkoani Mwanza, baada ya kufariki dunia ghafla.

Tukio la kuugua ghafla na kufikwa na umauti lilitokea Machi 29, mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Sengerema na kuzikwa Machi 31, mwaka huu katika Kijiji cha Bupandwamhela, huku mazishi yake yakihudhuriwa na familia ya mzee Bukumbi sambamba na ndugu jamaa na marafiki.

Kabla ya maziko kufanyika, kulitanguliwa na ibada iliyoongozwa na Mchungaji John Swakala wa Kanisa la Pentecostal la kijijini hapo. Baada ya kuzika, kaka wa marehemu, Eric Shigongo alitoa neno la shukrani kwa wote waliojitokeza kwenye msiba huo.

Pumzika kwa amani Daudi Zabron!
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!

Leave A Reply