The House of Favourite Newspapers

Putin Ataka Kuonana na Trump Baada ya Kuapishwa

Vladimir PutinRais wa Urusi, Vladimir Putin amesema ataonana na Rais mteule wa Marekani, Donald Trump mara tu atakapo apishwa kuingia madarakani mnamo Januari 20, 2017.

Putin amewaambia waandishi wa habari kuwa alimuunga mkono Trump ili kuweka sawa uhusiano wa Marekani na nchi yake.

483208412-real-estate-tycoon-donald-trump-flashes-the-thumbs-up-jpg-crop-promo-xlarge2Putin ameongeza kuwa halitakuwa jambo rahisi ukizingatia na namna nchi zote mbili zinavyotofautiana kimisimamo, lakini atafanya kila awezalo kuweka mambo sawa zaidi.

Juma lililopita, Shirika la upelelezi nchini Marekani CIA liliishutumu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani kwa kumuunga mkono Trump.

Darassa Afunguka Tuhuma za Kuiba Beat ya Saida Karoli Kwenye Wimbo Wake wa Muziki

Comments are closed.